Friday, November 2, 2012

MTU TAJIRI KULIKO WOTE DUNIANI ATAKA KUINUNUA GETAFE

Carlos Slim, mwanaume tajiri kuliko wote duniani

CARLOS Slim, ambaye anaamini kuwa mtu tajiri kuliko wote duniani, ameamua kununua kwenye Ligi Kuu ya Hispania, na kwa mujibu wa tovuti ya 'Libertad Digital', amepiga hatua ya kwanza kuelekea kuwa mmiliki mpya wa Getafe.

Angel Torres, mwenyekiti wa klabu hiyo, amekuwa akisaka mnunuzi kutokana na klabu hiyo kuelemewa na madeni, na tajiri huyo Mmexico anajiandaa kuinunua Getafe.

Carlos Slim ameanza mazungumzo ya kuinunua Getafe na dili linatarajiwa kukamilika ndani ya siku chache zijazo.

Tajiri huyo ni shabiki mkubwa wa soka la Hispania na anadhamiria kuibadili klabu hiyo kuwa moja ya klabu kubwa zaidi barani Ulaya. Pesa si kikwazo kwa sababu ana 'pochi' nene sana.

Ununuzi unatarajiwa kusimamiwa na kampuni ya America Movil, ambayo ina haki za kuonyesha mechi za ligi hiyo ya Hispania inayofahamika pia kama 'Liga BBVA' nchini Mexico.

Ndoto ya Carlos Slim ni kuiona Getafe inakuwa timu ya kupigania ubingwa na kuleta upinzani kwa Real Madrid na Barcelona.

No comments:

Post a Comment