Tuesday, November 13, 2012

MESSI AICHANGANYA BARCELONA KWA MSHAHARA MPYA ANAOUTAKA... WAO WAMTENGEA BILIONI 20/- KWA MWAKA... YEYE ATAKA WAMDAKISHE SH. BILIONI 30 KWA MWAKA.!

Lionel Messi
BARCELONA, Hispania
STRAIKA Lionel Messi amewastua viongozi wa Barcelona kutokana na ombi la kutaka alipwe mshahara mkubwa zaidi ndipo asaini mkataba mpya utakaomuongezea kipindi cha kuendelea kuichezea klabu yake hiyo.

Barca wamedhamiria kuongeza na kuboresha mkataba wa sasa wa Messi unaomalizika mwaka 2016 kabla ya kipindi cha sikukuu ya krismas.

Nyota huyo wa Argentina amepewa ofa ya mkataba wenye thamani ya euro milioni 10 kwa mwaka (Sh. bilioni 20), lakini kambi ya mchezaji huyo anayeshikilia tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia imeishangaza Barca kwa kutaka mshahara wa euro milioni 15 kwa mwaka (Sh. bilioni 30), kwa mujibu wa jarida la El Economista.

Taarifa hizo zimedai kuwa hadi sasa, Barca bado hawajajibu ombi hilo la kambi ya Messi.

No comments:

Post a Comment