|
Kiatu cha Lionel Messi wa Barcelona kikionekana na jina la mwanae aliyempa jina la THIAGO aliyezaliwa wikiendi iliyopita wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Celtic kwenye Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow, Scotland jana usiku. Barca walilala 2-1. Mkenya Victor Wanyama alifunga goli moja la Celtic na jingine lilifungwa na yosso mwenye umri wa miaka 18 aliyeingia kutokea benchi, Tony Watt. Goli la kufutia machozi ya Barca lilifungwa na Messi. Messi sasa amebakisha goli moja kuifikia rekodi ya gwiji wa Brazil, Pele, ya kufunga magoli 75 katika mwaka mmoja. Picha: REUTERS |
|
Lionel Messi wa Barcelona akishangilia goli lake kwa kunyonya kidole gumba kuashiria kuzaliwa kwa mwanae wa kwanza, THIAGO, wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Celtic kwenye
Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow, Scotland jana usiku. Barca
walilala 2-1. Mkenya Victor Wanyama alifunga goli moja la Celtic na
jingine lilifungwa na yosso mwenye umri wa miaka 18 aliyeingia kutokea
benchi, Tony Watt. Goli la kufutia machozi ya Barca lilifungwa na
Messi. Messi sasa amebakisha goli moja kuifikia rekodi ya gwiji wa
Brazil, Pele, ya kufunga magoli 75 katika mwaka mmoja. Picha: REUTERS |
|
RVP wewe ni jembeeee... kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson akiwapa dole wachezaji wake wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu dhidi ya Braga. Man U ilishinda 3-1 kupitia magoli ya Robin van Persie, Rooney (penalti) na Chicharito. |
|
Mchezaji wa Juventus, Alessandro Matri akimiliki mpira wakati wa mechi yao ya Kundi E la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Nordsjaelland kwenye Uwanja wa Juventus mjini Turin jana Novemba 7, 2012. Juve walishinda 4-0. Picha: REUTERS |
|
Utadhani siye Pirlo... kiungo 'jembe' la Juventus, Andrea Pirlo akipiga makofi baada ya mechi yao ya Kundi E la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Nordsjaelland kwenye Uwanja wa Juventus mjini Turin jana Novemba 7, 2012. Juve walishinda 4-0. Picha: REUTERS |
|
Mashine hiyo wanayoitaka Chelsea.... Willian wa Shakhatar akishangilia |
|
Willian wa Shakhatar |
|
Kiungo wa BATE Borisov, Alexandr Hleb (katikati) akilindwa na wachezaji wa Valencia, Ricardo Costa (kushoto) na Fernando Gago wakati wa mechi yao ya Kundi F la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Mestalla mjini Valencia, jana Novemba 7, 2012. Picha: REUTERS |
|
Mchezaji wa Shakhtar Donetsk, Tomas Hubschman (kulia) akimbana straika wa Chelsea, Fernando Torres wakati wa mechi yao ya Kundi E la Ligi ya Klabu Bingwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London Novemba 7, 2012. Picha: REUTERS |
|
Kocha wa Chelsea, Roberto di Mateo akitoa maelekezo |
|
Kiungo wa Juventus, Andrea Pirlo (kulia) akimuacha mchezaji wa Nordsjaelland, Mikkel Beckmann wakati wa mechi yao ya Kundi E la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Juventus mjini Turin jana Novemba 7, 2012. Juve walishinda 4-0. Picha: REUTERS |
|
Beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic akiwania mpira dhidi ya mchezaji wa Shakhtar Donetsk, Razvan Rat wakati wa mechi yao ya Kundi E la Ligi ya Klabu Bingwa
kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London
jana Novemba 7, 2012. Chelsea walishinda 3-2. Picha: REUTERS |
|
Winga wa Bayern Munich, Franck Ribery akionyeshwa kadi ya njano kwa kumlalamikia refa wa Romania, Ovidiu Alin Hategan (kulia) wakati akipumzishwa katika mechi yao ya Kundi F la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Lille mjini Munich Novemba 7, 2012. Bayern ilishinda 6-1. Picha: REUTERS |
|
Straika wa Benfica, Oscar Cardozo akishangilia goli lake la pili dhidi ya Spartak Moscow wakati wa mechi yao ya Kundi G la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Luz mjini Lisbon jana Novemba 7, 2012. Picha: REUTERS |
|
Beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic
akichezewa faulo na Willian wa Shakhtar Donetsk (kulia) wakati wa mechi yao ya Kundi E la Ligi ya Klabu Bingwa
kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London
jana Novemba 7, 2012. Chelsea walishinda 3-2. Picha: REUTERS |
|
Straika wa Barcelona, David Villa akijilaumu baada ya kukosa goli dhidi ya Celtic wakati wa mechi yao ya Kundi G la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow, Scotland jana Novemba 7, 2012. Picha: REUTERS |
|
Straika wa Barcelona, Lionel Messi (katikati) akijaribu kushuti golini huku akibanwa na mchezaji wa Celtic, Adam Mathews wakati wa mechi yao ya Kundi G la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow, Scotland jana Novemba 7, 2012. Picha: REUTERS |
|
Oscar Cardozo wa Benfica akishangilia baada ya kutupia |
|
Dah.... umenibania sana leo, siamini!!! Straika wa Barcelona, Lionel Messi (kushoto) akimuangalia kipa wa Celtic, Fraser Forster baada ya kuokoa shuti la Messi wakati wa mechi yao ya Kundi G la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow, Scotland jana Novemba 7, 2012. Picha: REUTERS |
|
Mchezaji wa Celtic, Kelvin Wilson (kulia) akimpa shughuli kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas wakati wa mechi yao ya Kundi G la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow, Scotland jana Novemba 7, 2012. Picha: REUTER |
|
Messi akishangilia goli lake kwa kunyonya dole gumba akiashiria kuzaliwa kwa mwanae wa kwanza aliyempa jina la Thiago wakati wa mechi yao dhidi ya Celtic. |
|
Sijaona Mkenya kama wewe uwanjani... Kocha wa Celtic, Neil Lennon (kushoto) akimpongeza mmoja wa wafungaji wa Celtic, Mkenya Victor Wanyama, baada ya ushindi wa timu yao dhidi ya Barcelona katika mechi ya Ligi ya Klabu
Bingwa dhidi ya kwenye Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow nchini
Scotland jana Novemba 7, 2012. Celtic ilishinda 2-1. Picha: REUTERS |
|
Mkenya Victor Wanyama
wa Celtic (kushoto) akipongezwa na wenzake baada ya kufunga goli dhidi ya
Barcelona wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya jana. Picha:
Reuters |
|
Messi akimpiga chenga Wanyama |
|
Winga wa Chelsea, Victor Moses (kushoto)
akishangilia na mchezaji wenzake Gary Cahill (kulia) baada
ya kufunga goli wakati wa mechi yao ya Kundi E la Ligi ya Klabu Bingwa
dhidi ya Shakhtar Donetsk kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London
jana Novemba 7, 2012. Chelsea walishinda 3-2. Picha: REUTERS |
|
Winga wa Chelsea, Victor Moses (kushoto)
akishangilia na mchezaji wenzake Gary Cahill (kulia) baada
ya kufunga goli wakati wa mechi yao ya Kundi E la Ligi ya Klabu Bingwa
dhidi ya Shakhtar Donetsk kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London
jana Novemba 7, 2012. Chelsea walishinda 3-2. Picha: REUTERS |
|
Winga wa Chelsea, Victor Moses (katikati)
akishangilia na wachezaji wenzake Gary Cahill (kulia) na Juan Mata baada
ya kufunga goli wakati wa mechi yao ya Kundi E la Ligi ya Klabu Bingwa
dhidi ya Shakhtar Donetsk kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London
jana Novemba 7, 2012. Chelsea walishinda 3-2. Picha: REUTERS |
|
Winga wa Chelsea, Victor Moses (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake Gary Cahill (kulia) na Juan Mata baada ya kufunga goli wakati wa mechi yao ya Kundi E la Ligi ya Klabu Bingwa dhidi ya Shakhtar Donetsk kwenye Uwanja wa Stamford Bridge mjini London jana Novemba 7, 2012. Chelsea walishinda 3-2. Picha: REUTERS |
|
Straika wa Manchester United, Wayne Rooney (kushoto) akipongezwa na mchezaji mwenzake Robin van Persie baada ya kufunga dhidi ya Braga wakati wa mechi yao ya Kundi H la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Manispaa mjini Braga, jana Novemba 7, 2012. Man Utd ilishinda 3-1. REUTERS |
|
Yosso wa Celtic, Tony Watt (kulia) akifunga goli dhidi wa kipa wa Barcelona, Victor Valdes wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa kwenye Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow nchini Scotland jana Novemba
7, 2012. Celtic ilishinda 2-1. Picha: REUTERS |
|
Kocha wa Celtic, Neil Lennon, akishangilia ushindi wa timu yake dhidi ya Barcelona baada ya mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa dhidi ya kwenye Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow nchini Scotland jana Novemba 7, 2012. Celtic ilishinda 2-1. Picha: REUTERS |
|
Wachezaji wa Celtic wakimpongeza Tony Watt (32) kwa goli alilofunga wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow nchini Scotland jana Novemba 7, 2012. Celtic walishinda 2-1. Picha: REUTERS |
|
Nimetishaaa.... yosso wa Celtic, Tony Watt (kulia) akishangilia goli lake wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa dhidi ya Barcelona kwenye Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow nchini Scotland jana Novemba 7, 2012. Picha: REUTERS |
Matokeo na misimamo ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya mechi za jana na juzi:
KUNDI E
Juventus 4 Nordsjaelland 0
Chelsea 3 Shakhtar Donetsk 2
Msimamo P W D L F A Pts
Shakhtar Donetsk 4 2 1 1 7 5 7
Chelsea 4 2 1 1 10 6 7
Juventus 4 1 3 0 8 4 6
Nordsjaelland 4 0 1 3 1 11 1
KUNDI F
Valencia 4 BATE Borisov 2
Bayern Munich 6 Lille 1
Msimamo P W D L F A Pts
Bayern Munich 4 3 0 1 10 5 9
Valencia 4 3 0 1 10 4 9
BATE Borisov 4 2 0 2 8 9 6
Lille 4 0 0 4 2 12 0
KUNDI G
Benfica 2 Spartak Moscow 0
Celtic 2 Barcelona 1
Msimamo P W D L F A Pts
Barcelona 4 3 0 1 8 5 9
Celtic 4 2 1 1 6 5 7
Benfica 4 1 1 2 3 4 4
Spartak Moscow 4 1 0 3 6 9 3
KUNDI H
CFR Cluj 1 Galatasaray 3
Braga 1 Manchester United 3
Msimamo P W D L F A Pts
Manchester United * 4 4 0 0 9 4 12
Galatasaray 4 1 1 2 4 5 4
CFR Cluj 4 1 1 2 5 6 4
Braga 4 1 0 3 5 8 3
* Inaonyesha timu iliyosonga mbele hatua ya mtoano
Zilizochezwa juzi Jumanne
KUNDI A
Dynamo Kiev 0 Porto 0
Paris St Germain 4 Dinamo Zagreb 0
Msimamo P W D L F A Pts
Porto * 4 3 1 0 6 2 10
Paris St Germain 4 3 0 1 10 2 9
Dynamo Kiev 4 1 1 2 5 7 4
Dinamo Zagreb 4 0 0 4 0 10 0
* Inaonyesha timu iliyosonga mbele hatua ya mtoano
Kundi B
Schalke 04 2 Arsenal 2
Olympiakos Piraeus 3 Montpellier HSC 1
Msimamo P W D L F A Pts
Schalke 04 4 2 2 0 8 5 8
Arsenal 4 2 1 1 7 6 7
Olympiakos Piraeus 4 2 0 2 7 7 6
Montpellier HSC 4 0 1 3 5 9 1
KUNDI C
Anderlecht 1 Zenit St Petersburg 0
AC Milan 1 Malaga 1
Msimamo P W D L F A Pts
Malaga * 4 3 1 0 8 1 10
AC Milan 4 1 2 1 4 4 5
Anderlecht 4 1 1 2 1 4 4
Zenit St Petersburg 4 1 0 3 3 7 3
* Inaonyesha timu iliyosonga mbele hatua ya mtoano
Kundi D
Manchester City 2 Ajax Amsterdam 2
Real Madrid 2 Borussia Dortmund 2
Msimamo P W D L F A Pts
Borussia Dortmund 4 2 2 0 6 4 8
Real Madrid 4 2 1 1 10 7 7
Ajax Amsterdam 4 1 1 2 6 8 4
Manchester City 4 0 2 2 6 9 2
No comments:
Post a Comment