Saturday, November 17, 2012

MAN CITY YAKAA KILELENI KWA MARA YA KWANZA MSIMU HUU, MASHETANI YAANGUKIA PUA, CHELSEA NAYO CHALI, ARSENAL, LIVERPOOL ZAUA

Wachezaji wa Arsenal wakimpongeza Walcott (kulia) baada ya kufunga dhidi ya Tottenham leo.
Luis Suarez akishangilia goli lake. Jamaa sasa amekaa kileleni mwa orodha ya wafungaji wanaoongoza akiwa na mabao 10
Goooooo! Kipa Anders Lindegaard wa Man Utd akiruka bila ya mafanikio wakati mpira ukitinga wavuni dhidi ya Norwich City leo
Peter Odemwingie (kushoto) na Morrison (kulia) wakimpongeza Shane Long (katikati) kwa goli alilofunga dhidi ya Chelsea.

SERGIO Aguero na Carlos Tevez walifunga mara mbili kila mmoja wakati Manchester City ilipotoa kipigo cha mbwa mwizi kwa Aston Villa cha mabao 5-0 kwa na kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza msimu huu leo.

Katika siku ambayo hapakuwa na matokeo ya sare, Man United ililala isivyotarajiwa 1-0 ugenini dhidi ya Norwich, Arsenal iliifunga iliifunga Tottenham 5-2, Liverpool ikashinda 3-0 dhidi ya Wigan, Chelsea ikalala 2-1 kwa West Brom, Everton ikapigwa 2-1 na Reading, Newcastle nayo ilitoka hoi kwa kulala 2-1 nyumbani dhi dhidi ya Swansea.

Pata matokeo kamili ya mechi za leo za Ligi Kuu ya England:Played GD   Pts
 1 Man City 12 15 28
2 Man Utd 12 12 27
3 Chelsea 12 11 24
4 West Brom 12 6 23
5 Everton 12 6 20
6 Arsenal 12 10 19
7 West Ham 11 3 18
8 Tottenham 12 -1 17
9 Fulham 11 5 16
10 Swansea 12 2 16
11 Liverpool 12 1 15
12 Newcastle 12 -4 14
13 Norwich 12 -9 14
14 Stoke 11 -1 12
15 Wigan 12 -9 11
16 Sunderland 10 -4 9
17 Reading 11 -5 9
18 Aston Villa 12 -12 9
19 Southampton 12 -12 8
20 QPR 12 -14 4

No comments:

Post a Comment