Saturday, November 17, 2012

JACKSON MAKWETA AFARIKI DUNIA... NI WAZIRI WA ZAMANI KATIKA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA... ALIANDIKA REKODI KWA KUSHIKILIA UBUNGE JIMBO LA NJOMBE KASKAZINI KUANZIA MWAKA 1975 HADI MWAKA 2010 ALIPONG'OLEWA NA DEO SANGA

Jackson Muvangila Makweta enzi za uhai wake
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Njombe Kaskazini na Waziri wa zamani wa Elimu na wizara nyingine mbalimbali katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jackson Makweta, amefariki dunia leo baada ya kuugua.

Taarifa zilizothibitishwa leo zimedai kuwa Makweta amefariki baada ya kuugua maradhi ya ini na figo na kulazwa katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi Lugalo na kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Ijumaa kabla hajafariki dunia leo Jumamosi (Novemba 17) mishale ya saa 11:00 jioni. 
Taarifa zimedai kuwa awali, marehemu alianza matibabu katika Hospitali ya Ikonda mkoani Iringa kabla ya kuhamishiwa jijini Dar es Salaam.

Shughuli za mazishi zinaendelea kufanyika nyumbani kwake Goba kwa Wagogo jijini Dar es Salaam.  

Makweta aliyezaliwa miaka 69 iliyopita, alikuwa ni miongoni mwa watu wachache waliokuwa wakishikilia rekodi ya kudumu na cheo cha ubunge kwa muda mrefu nchini kwani aliingia madarakani mwaka 1975 na kung'olewa mwaka 2010.


Mungu aiweke pema roho ya marehemu.

1 comment: