Wednesday, November 21, 2012

MAN CITY WAMESHATOLEWA ULAYA - MOURINHO

Jose Mourinho
Roberto Mancini


KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho anaamini kwamba Manchester City tayari wameshatolewa nje ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Man City wanaikaribisha timu ya Mourinho leo huku wakifahamu kwamba ni lazima washinde mechi zao mbili zilizobaki ili kuwa na uwezekano wa kusonga mbele katika hatua ya 16-Bora.

Lakini Mourinho alisema: "Nadhani wanaweza kushinda kesho (leo), ni kweli wanaweza, na wanaweza kushinda ugenini dhidi ya Dortmund, kwanini wasiweze, lakini pointi nane hazitoshi.

"Nadhani wameshatolewa kwa mara ya pili na jambo gumu kwao."

Mourinho atakuwa kocha kijana zaidi kuiongoza timu katika mechi 100 za Ligi ya Klabu Bingwa leo na kocha wa tano tu kufikisha idadi hiyo ya mechi baada ya Carlo Ancelotti, Arsene Wenger, Ottmar Hitzfeld na Sir Alex Ferguson. 


Licha ya kuamini kwamba watatolewa mapema, Mourinho amesema Man City wana kikosi kinachoweza kutwaa ubingwa wa Ulaya miaka ijayo.

No comments:

Post a Comment