Thursday, November 1, 2012

KAKA ANG'ARA NA KUTUPIA MOJA WAKATI REAL MADRID IKISHINDA 4-1 KOMBE LA MFALME DHIDI YA ALCOYANO...!

Kaka akipongezwa na wachezaji wenzake wa Real Madrid baada ya kufung goli katika mechi yao ya Kombe la Mfalme usiku wa jana (Oktoba 31, 2012) kuamkia leo.
safiiii...! Kaka akishangilia bao alilofunga jana.
Kaka na wenzake wakimpongeza Benzema baada ya kufunga goli dhidi ya Alcoyano jana Oktoba 31, 2012.
Kaka na wenzake wakimpongeza yosso José Rodríguez (Na. 34) baada ya kufunga goli katika mechi yao ya Kombe la Mfalme dhidi ya Alcoyano jana Oktoba 31, 2012.
MADRID, Hispania
REAL Madrid ni kama imeshajihakikishia kucheza hatua ya robo fainali ya Kombe la Mfalme baada ya kushinda ugenini 4-1 dhidi ya Alcoyano huku kiungo wake wa kimataifa wa Brazil, Kaka akionyesha kiwango cha juu na kufunga bao moja usiku wa kuamkia leo.

Karim Benzema alifunga goli la utangulizi na Kaká akaongeza la pili kabla ya mapumziko. Yosso José Rodríguez alifunga la tatu na Benzema akaongeza jingine wakati wenyeji wakipata bao lao la kufutia machozi kupitia kwa Javi Lara.

Katika mechi hiyo, Real walichezesha yosso wengi katika kikosi kilichoanza ambao ni pamoja na Nacho Fernández, Álex Fernández na Álvaro Morata.

No comments:

Post a Comment