Tuesday, November 13, 2012

DEMBA BA AJITOA TAIFA SENEGAL

Demba Ba

DAKAR, Senegal
MSHAMBULIAJI wa Newcastle United, Demba Ba ni miongoni mwa wachezaji sita wa kikosi cha kwanza waliojitoa kwenye kikosi cha Senegal kitakachocheza mechi ya kirafiki nchini Niger kesho, shirika la habari la Agence Presse Senegalaise lilisema jana.


Ba aliichezea Newcastle katika mechi yao ya ligi kuu nyumbani dhidi ya West Ham juzi Jumapili bila ya kuwa na majeraha yoyote yanayoonekana lakini anaungana na Lamine Sane (Bordeaux), Cheikh Mbengue (Toulouse), Pape Ndiaye Souare (Stade Reims), Idrissa Gana Gueye (Lille) na Issiar Dia anayechezea klabu ya Qatar ya Lekhwiya, katika orodha ya watakaokosa mechi hiyo.


Kocha wa muda wa Senegal, Mayacine Mar ameziba mapengo yao kwa kuwaita Ibrahima Ba (Istres), Malick Mane (Sogndal) na Pape Alioune Diouf (Kalmar).


Senegal imekosa kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwezi uliopita baada ya mechi yao dhidi ya Ivory Coast mjini Dakar kuvunjwa kutokana na vurugu za mashabiki.

No comments:

Post a Comment