Saturday, November 17, 2012

CARLOS TEVEZ APATA SOO LA MWAKA... ETI LICHA YA KULIPWA SH. MILIONI 500 KILA WIKI ASHINDWA KULIPIA LESENI YA GARI LAKE LA BEI MBAYA AINA YA PORSCHE NA KUJIKUTA AKIADHIRIWA NA POLISI USIKU KUAMKIA JANA BAADA YA KUPIGWA BAO NA GARI HILO KUBEBWA MSOBEMSOBE NA KWENDA KUSWEKWA YADI ZA TRAFIKI

Gari la Tevez likiondoshwa na trafiki baada ya straika huyo 'kupigwa bao' wakati akitoka mazoezini.

Tevez... anavyoonekana baada ya gari lake kupigwa bao na kisha kupelekwa polisi na 'winchi'

Hapa Tevez akijifua na wachezaji wenzake wa Man City kabla ya kupigwa bao na trafiki wakati akielekea nyumbani kwake

MANCHESTER, England
Carlos Tevez alikumbana na kimbembe cha polisi usiku wa kuamkia jana baada ya kusimamishwa na kukamatwa kwa gari lake lililobebwa msobemsobe na polisi kwa kushindwa kulipia leseni yake.

Tevez alisimamishwa na 'trafiki' wakati akiendesha gari lake jipya jeupe aina ya Porsche Panamera jijini Manchester.

Hadi sasa, Tevez amekuwa akiendesha gari kwa kutumia leseni ya kimataifa, licha ya kuambiwa miezi 12 iliyopita kwamba anapaswa kulipia na kupata leseni halali ya kuendesha gari nchini Uingereza.

Straika huyo wa Argentina baadaye alilazimika kutolewa ndani ya gari hilo na kushuhudia 'mkoko' wake wa bei mbaya ukibebwa msobemsobe na 'winchi'.

Hata hivyo, polisi wa jiji la Manchester wameanza harakati za kumsaidia kukamilisha taratibu, lakini kwa sasa, gari la Tevez linaendelea kushikiliwa kwenye yadi za polisi.

Man City walipinga vikali madai kwamba Tevez alikamatwa, lakini gazeti la Sportsmail liliripoti kwamba straika huyo wa Argentina anakabiliwa na adhabu ikiwamo ya faini.

Tevez, ambaye hulipwa na Man City mshahara wa wiki wa paundi za England 200,000 (Sh. bilioni 500), ni shabiki mkubwa wa magari yaendayo kasi, hasa hili lililokamatwa la Porsche -- ambalo kulinunua lilimgharimu paundi za England 120,000 (Sh. milioni 300)

Alirejea mazoezini jana wakati akisubiri kujua kama atapewa adhabu nyingine zaidi. Wakati akirejea nyumbani kwake kutoka mazoezini, Tevez alionekana akichangamkia 'lifti' katika gari jingine aina ya Porsche.

No comments:

Post a Comment