Saturday, November 24, 2012

SOMA ALICHOSEMA SAID FELLA BAADA YA BIBI CHEKA KUTANGAZWA KWENYE CITIZEN TV YA KENYA KISHA KUITWA NI MKENYA... DOGO ASLAY PIA AITWA MKENYA KORA AWARDS

 
http://www.ghafla.co.ke/news/music/item/4911-mind-blowing-kenyan-grandmother-doing-a-freestyle-rap-in-the-village
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Bibi Cheka, wa familia ya Mkubwa na Wanae inayoongozwa na Said Fella, ametangazwa kama msanii wa Kenya baada ya habari yake kuripotiwa katika kituo cha televisheni cha Kenya cha Citizen TV (ANGALIA VIDEO HIYO HAPO JUU pia CLICK LINK HIYO CHINI YA VIDEO).
Katika ripoti hiyo mtangazaji anasikika akisema kwamba Bibi Cheka mwenye umri wa miaka 51 ni msanii wa kikundi cha mitaani alichokutwa akiimba nacho.
Video iliyochukuliwa kutoka katika ripoti ya Citizen TV ya Kenya imezagaa kwenye mitandao ikimuonyesha msanii huyo kutoka Temeke akiimba 'freestyle' mtaani huku mitandao akimnadi kama Mkenya.
Tukio hilo limekuja siku chache tu tangu msanii mwingine wa familia ya Mkubwa na Wanae, Dogo Aslay, kutajwa katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo ya Kora, akitambulishwa kama Mkenya.
Bosi wa familia ya Mkubwa na Wanae, Fella ameiambia STRAIKA leo kuwa anashangazwa na mambo yanayoendelea.
"Sijui ni nani anayefanya mambo haya... tunatumia nguvu nyingi kuwatengeneza wasanii hawa lakini anaibuka mtu na kupotosha taarifa zinazowahusu. Bibi Cheka na Aslay si Wakenya," alisema Mkubwa Fella.  
  Alisema asili ya wazazi wa Bibi Cheka ni Morogoro na Mbeya, wakati Dogo Aslay wazazi wake ni mchanganyiko wa Mzaramo na Mndengereko.
"Si Wakenya hawa ni Watanzania," alisisitiza Fella huku akisema anafirikia hatua za kuchukua kuhusiana na suala hilo.  
 

No comments:

Post a Comment