Friday, November 23, 2012

BENITEZ: SIJAAJIRIWA NA ROMAN ABRAMOVICH CHELSEA KWA SABABU TU YA FERNANDO TORRES... ATUA MAZOEZINI NA KUANZA KAZI YAKE MARA MOJA... ASEMA KINA FERNANDO TORRES, OSCAR, RAMIRES WATATISHA MBAYA!

Nimefurahi sana kuungana tena na Fernando Torres...! Rafael Benitez akionyesha jezi yake katika klabu ya Chelsea baada ya kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari leo Novemba 22, 2012.
Benitez akipelekwa kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu yake mpya ya Chelsea leo.
Benitez akitua Chelsea

Sijui nitafikisha mechi 10? Anyway... hapa nimefuata mkwanja tu ...! hapa tayari keshatupia nguo za kazi na kuanza kazi ya kuifundisha Chelsea kwa mara ya kwanza leo Novemba 22, 2012.
Nahodha John Terry wa Chelsea akielekea mazoezini na mkoko wake wa bei mbaya leo

Fernando Torres wa Chelsea akielekea mazoezini leo Novemba 22, 2012.
Hayaaa...! Anzeni kujifua sasa niwaone

Benitez akitoa maelekezo muhimu kwa straika Fernando Torres na mwenzake wakati wa mazoezi yao leo Nov. 22, 2012.

Sasa nitatisha tena kama nilivyokuwa Liverpool....!  Torres akikokota mpira mbele ya kocha wake Rafael Benitez wakati wakiwa kwenye mazoezi yao leo Novemba 22, 2012.   
Hatukutaki...! Baadhi ya mashabiki wa Chelsea wakiandamana kupinga ujio wa kocha Rafael Benitez katika klabu yao leo Nov.22, 2012. 

Rafa nje...! Shabiki mmoja wa Chelsea akionyesha bango lake kupinga kuajriwa kwa Rafael Benitez 
LONDON, England
Kocha wa muda wa Chelsea, Rafael Benitez amesisitiza kwamba hajaajiriwa na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kwa sababu tu ya kufufua kiwango cha straika Fernando Torres na amedai kwamba Mhispania huyo aliyenunuliwa kwa paundi za England milioni 50 (Sh. bilioni 130) yuko 'fiti' kurejesha tena makali yake akiwa Stamford Bridge.

Torres anamsifu Benitez kwa kumfanya awe mmoja wa mastraika bora duniani wakati wa kipindi chake cha kuwa kwenye kiwango cha juu kwenye klabu ya Liverpool na kocha huyo aliyemrithi tRoberto Di Matteo katika klabu ya Chelsea ianaamini kuwa kukutana tena kwa wawili hao kunaweza kuleta mafanikio kama ilivyokuwa Anfield.

"Nilijua kila mmoja atazungumza kuhusu," alisema Benitez wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi uliofurika kuliko kawaida.

"Kila mmoja anazungumzia kuhusu yeye (Torres) kutofanya vizuri akiwa Chelsea, lakini wakati nilipoangalia mechi, mara zote niliamini kwamba amekuwa katika mwelekeo mzuri sana. Kwenye mazoezi leo, alionyesha kuwa katika hali nzuri na kwa pamoja, tunaweza kufanya mambo makubwa kwa klabu hii.

"Hili si suala la Fernando tu. Fernando ni mchezaji wa kiwango cha juu na ataimarika kama wengine. Nitasema nimewaona wachezaji wengi mazoezini. Oscar, Ramires, (Cesar) Azpilicueta, nawaona wakiwa katika hali nzuri sana.

"Tunaweza kuwasaidia waimarike? Tutajitahidi kufanya kila tunachoweza. Najua ni kwa namna gani wachezaji wote wanaweza kuwa wazuri. Fernando ni mmoja wa wachezaji muhimu katika timu hii. Nitajitahidi kumuinua kiwango chake kama nitakavyowainua wengine wote."

No comments:

Post a Comment