Tuesday, October 2, 2012

WAREMBO REDDS MISS TANZANIA WAANZA KAMBI GIRAFFE HOTEL LEO

Washiriki Redds Miss Tanzania 2012 wakijichana misosi baada ya kuwasili kambini kwenye hoteli ya Giraffe jijini Dar es Salaam leo
 




Vimwana wa Redds Miss Tanzania 2012 wakipata maelekezo kutoka kwa mfanyakazi wa hoteli ya Giraffe, James Philbert baada ya kuwasili kuanza kambi katika hoteli hiyo leo

WASHIRIKI wa fainali za taifa za urembo mwaka huu 'Redd's Miss Tanzania 2012' wametakiwa kuwa na nidhamu wakati wote watakapokuwa kambini wakijiandaa na shindano hilo litakalofanyika mapema mwezi ujao jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na warembo hao leo baada ya kuwasili kambini, mratibu wa shindano hilo, Hashim Lundenga, aliwaambia washiriki hao kuwa kila mmoja anawajibika kumuheshimu mwenzake na hakuna aliye na thamani kubwa kuliko mwingine.


Lundenga aliwaambia warembo hao wawe wanajitambua na hilo litawajenga katika maisha yao na kuwatakia waishi kwa furaha katika muda wote watakaokuwa kwenye kambi hiyo.


"Karibuni wote hapa kwenye hoteli hii ambayo itakuwa ndio makazi yenu katika kuelekea shindano la Redd's Miss Tanzania, ila tambueni kwamba nyote mko sawa na kikubwa ni kuwa na nidhamu," alisisitiza mratibu huyo.


Aliwaambia warembo hao kwamba wakiwa kwenye kambi hiyo watafundishwa mambo mbalimbali yanayohusiana na sanaa ya urembo, kujiandaa na maisha na kujitambua.


Aliwataja warembo hao waliongia kambini leo kuwa ni Noela Michael, Magdalena Roy, Mary Chizi, Naomi Jones, Carren Elias, Venancy Edward, Warid Frank, Anande Raphaely, Lucy Stephano, Rose Lucas, Irene Veda, Joyce Baluhi, Virginia Mokiri, Fatma Twahil, Phina Revocatus, Belinda Mbogo, Lightness Michael, Elizabeth Diamond, Bridgitte Alfred, Diana Hussein na Irene David.


Aliwataja washiriki wengine kuwa ni Zuwena Nassib, Edda Sylivester, Flavia Maeda, Catherine Masumbigana, Jesca Haule, Eugene Fabian, Happiness Daniel, Happiness Rweyemamu na Babylove Kalalaa.


Mrembo anayeshikilia taji la mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Nchini (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's ni Salha Israel aliyetokea Kanda ya Ilala jijini.

No comments:

Post a Comment