Monday, October 29, 2012

REFA ALIYEINYONGA CHELSEA WAKATI MAN U IKISHINDA 3-2 DHIDI YA CHELSEA JANA AANZA KUKIONA CHA MOTO.. ATOSWA KATIKA ORODHA YA MAREFA WATAKAOCHEZESHA KATIKA LIGI KUU YA ENGLAND WIKI HII... CHAMA CHA SOKA ENGLAND CHAANZA UCHUNGUZI MKALI PIA DHIDI YAKE...!

Mark Clattenburg
LONDON, England
Chama cha Soka cha England (FA) kimeanza uchunguzi mkali baada ya klabu ya Chelsea kumtuhumu refa Mark Clattenburg kutumia "lugha chafu" dhidi ya wachezaji wake wawili wakati timu hiyo ikipata kipigo cha mabao 3-2 katika mechi yao ya Ligi Kuu ya England jana Jumapili.

"FA imeanza uchunguzi kuhusiana na tuhuma dhidi yake baada ya mechi ya Jumapili kwenye Uwanja wa Stamford Bridge kati ya Chelsea na Manchester United," imesema FA katika taarifa yake leo kupitia tovuti (www.thefa.com).

Tukio hilo linaelekea kutikisa soka la England, ambalo limetoka kupumua hivi karibuni kutokana na kashfa ya ubaguzi iliyosababisha kufungiwa kwa nahiodha wa Chelsea, John Terry.

Ilitangazwa pia jana kuwa Clattenburg ambaye ni refa huyo wa FIFA hatapangwa katika orodha ya marefa watakaochezesha mechi za Ligi Kuu ya England wiki hii.



Licha ya kutuhumiwa kuwatolea lugha chafu wachezaji wa Chelsea, Mark Clattenburg analaumiwa pia kwa kuwatoa kwa kadi nyekundu wachezaji Branislav Ivanovic na Fernando Torres kabla ya kuruhusu goli lililoonekana kuwa la "off side" kutoka kwa Javier Hernandez "Chicharito" na hivyo kuirahisishia Man U kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Chelsea jana.

No comments:

Post a Comment