Tuesday, October 23, 2012

MKENYA WANYAMA ETI NDIYE ANAYEAMINIWA NA CELTIC KUMSTOPISHA 'JINI' LIONEL MESSI WAKATI TIMU YAKE YA CELTIC ITAKAPOVAANA NA BARCELONA KATIKA MECHI YAO YA LIGI YA KLABU BINGWA ULAYA LEO USIKU SAA 3:45...!

Mleteni huyo Messi...! Victor Wanyama wa Celtic akishangilia baada ya kutupia bao katika mechi ya Ligi Kuu ya Scotland hivi karibuni.

Victor Wanyama


Victor Wanyama wa Celtic akishangilia baada ya kufunga goli la pili dhidi ya Helsingborgs IF wakati wa mechi ya kuwania kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Celtic Park, Agosti 29, 2012 mjini Glasgow, Scotland.
SCOTLAND
Straika wa zamani wa Celtic, John Hartson anaamini kwamba kiungo wa kimataifa wa Kenya, Victor Wanyama ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kumzima 'jini' Lionel Messi wakati watakaposhuka dimbani leo kucheza dhidi ya Barcelona katika mechi ya Kundi G la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Nou Camp.

Hartson anaamini kwamba Wanyama ambaye ni ndugu yake Mkenya mwingine, McDonald Mariga, ni kiungo mzuri na anaweza kumzuia Messi kama ilivyokuwa enzi zake mwaka 2004 wakati walipocheza dhidi ya Barca na kupata sare ya 1-1 baada ya kumdhibiti vyema Mbrazil Ronaldinho aliyekuwa ndiye Messi wa wakati huo.

“Ni kazi ngumu sana kumchunga mchezaji mmoja wakati mnapocheza dhidi ya timu kali kama ya Barca, lakini wakati tukienda pale, kulikuwa na Ronaldinho ambaye ndiye aliyekuwa Mwanasoka Bora Na. No duniani,” amesema Hartson.

“Alikuwa ndiye Messi wa wakati huo na Martin O’Neill alimpa majukumu Joos Valgaeren kumchunga wakati wote.

“Joos alikuwa akikimbia naye kila anakokwenda kama suti mwilini na Ronaldinho hakupata nafasi ya kupiga shuti.

“Mnaweza kufanya hivyo pia dhidi ya Messi? Mngeulizwa swali hilo pia wakati wa enzi za Ronaldinho, lakini mbinu hiyo ilitusaidia. Nadhani Wanyama anaiweza kazi hii.

“Sijui ni kitu gani atakachokifanya Lenny. Nadhani atatumia mtindo wa 4-5-1 huku Wanyama akikaa mbele ya beki namba nne kwa ajili ya kusaidia ulinzi.

“Wanyama ana umbo kubwa, ana nguvu, anaweza kunyang'anya mipira na kukimbia nayo. Ni mchezaji mwenye nguvu sana na pia anacheza kwa ushirikiano. Ni mkimbiaji mzuri pia na anacheza kwa kiwango cha juu.”

No comments:

Post a Comment