Monday, October 15, 2012

MAMIA MWANZA WAUAGA MWILI WA KAMANDA BARLOW … KUAGWA TENA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO KUANZIA SAA 5:00 ASUBUHI KWENYE KANISA LA MTAKATIFU AUGUSTINE UKONGA… RAIS KIKWETE ASTUSHWA… ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAMATA WAUAJI MARA MOJA..!


Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Liberatus Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo. 
Polisi wakiwa na jeneza la mwili wa marehemu Kamanda Barlwo kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo.

Baadhi ya waombolezaji waliofika kuuaga mwili wa marehemu Kamanda Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo.

Gari lililobeba mwili wa marehemu Kamanda Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo.Waziri William Lukuvi akitoa heshima zake za mwisho wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Kamanda Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo.

Waombolezaji wakiendelea kuuaga mwili wa marehemu Kamanda Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo.

Kwaheri Kamanda Barlow...!

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndikilo akihutubia waombolezaji wakati wa kuuaga mwili wa Kamanda Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo.

DCI Manumba (wa pili kutioka kulia, mbele) akiwa katika shughuli ya kuuaga mwili wa Kamanda Barlow kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo.
Mwalimu Dorothy Moses, aliyekuwa na marehemu wakati wa tukio

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi ni miongoni mwa viongozi mbalimbali waliojitokeza leo kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza kuuaga mwili wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Liberatus Barlow aliyeuawa usiku wa kuamkia juzi Jumamosi kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.

Mamia ya wananchi walihudhuria kuagwa kwa mwili wa kamanda huyo ambao ulisafirishwa kwa ndege jioni hii kuelekea jijini Dar es.

Waziri Lukuvi alisema kuwa Jeshi la Polisi liko imara na kwamba makamanda wengine wataendeleza jitihada za marehemu (Kamanda Barlow) katika kupambana na uhalifu bila kuchoka.   

Kwa mujibu wa ratiba, mwili wa Kmanda Barlow jijini Dar es Salaam kesho saa tano asubuhi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Augustine Ukonga kabla ya kwenda kuzikwa nyumbani kwao, Vunjo  mkoani Kilimanjaro.

DCI ROBERT MANUMBA
Akizungumza katika shughuli kuuaga mwili huo jijini Mwanza leo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, DCI Robert Manumba, alisema kuwa hadi sasa wamefikia hatua nzuri katika upelelezi wao kutokana na ushirikiano wanaupata kwa wananchi na kwamba wauaji ni lazima watapatikana.

Wengine waliozungumza mbele ya waombolezaji ni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Phillip Kalangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Salum Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Lenard Paul na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Anthony Ruta.

Kamanda Barlow aliuawa usiku wa kuamkia juzi (Jumamosi) kwa kupigwa risasi usiku wa kuelekea saa 8:00 baada ya kumfikisha mwanamke aliyempa lifti kwenye gari yake binafsi baada ya kumalizika kwa kikao cha harusi, Mwalimu Doroth.

Rais Jakaya Kikwete ametuma salam za rambirambi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspeka Jenerali Saidi Mwema, kuhusiana na kifo cha Kamanda Barlow na kuagiza jeshi hilo kuwakamata wahusika na kuwafikisha mbele ya mkono wa sheria.

No comments:

Post a Comment