Monday, October 1, 2012

ANZHI YA KINA SAMUEL ETO'O YAMFUKUZIA KAKA

Kaka wa Real Madrid (katikati) akijaribu kuwatoka Carlos Marchena wa Deportivo Coruna (kushoto) na kipa Daniel Aranzubia wakati wa mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid, jana Septemba 30, 2012.
(Picha: REUTERS)
MOSCOW, Urusi
Wakala wa Urusi, Shumi Babaev amethibitisha kwamba klabu tajiri ya Anzhi inayoshiriki Ligi Kuu ya Urusi inajiandaa kumtwaa Kaka na kumsajili wakati wa dirisha dogo la usajili wa Januari.

"Anzhi imefikiria kumtwaa Kaka kwa muda mrefu, hata hivyo, yeye si aina ya wachezaji ambao wanaweza kusajiliwa kirahisi. Tunaweza kuzungumzia ujio wake kwa uhakika wakati wa kipindi cha soko la usajili," amesema Babaev.Kaka alicheza jana wakati Real Madrid ilipocheza dhidi ya Deportivo Coruna katika La Liga, Ligi Kuu ya Hispania ambayo walishinda 5-1.

Hivi sasa, Anzhi ambayo tayari ina "majembe" kadhaa kikosini kama Eto'o, Christopher Samba na Lassana Diara, ndiyo inayoongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Urusi na kuwapiku vigogo CSKA Moscow, Lokomotov na Zenit St. Petersburg.

No comments:

Post a Comment