Tuesday, September 18, 2012

WACHEZAJI REAL MADRID WALIBWATUKIANA BAADA YA KUCHAPWA NA SEVILLA

Kipa wa Real Madrid, Iker Casillas akiingia uwanjani wakati wa mechi ya La Liga dhidi ya Sevilla kwenye Uwanja wa Estadio Ramon Sanchez Pizjuan mjini Seville, Hispania Septemba 15, 2012.  Real walipigwa 1-0. 

WACHEZAJI wa Real Madrid walishukiana vikali wakati wakielekea kwenye chumba cha kuvalia baada ya kipigo kutoka kwa Sevilla Jumamosi.

Tovuti ya grada360.com imesema sauti za juu zilisikika kutoka kwa wachezaji wa Real na Jose Mourinho wakati wakiwa katika njia ya kuelekea kwenye chumba cha kuvalia baada ya mechi.

Mourinho alikuwa wa kwanza kubwatuka.

"Naenda kwenye mkutano na waandishi wa habari. Sitamtetea yeyote kati yenu! Kwa sababu hamkuwa tayari kunionyesha sura zenu uwanjani, nitajitetea mimi tu," aliwaka, kabla ya kuondoka kutoka katika chumba cha kuvalia.

Kisha wachezaji nao wakaanza kubwatuka.

"Vipi jamani, kimetutokea nini? (...) Sisi Real Madrid!" alisema Iker Casillas.

Hakuna aliyejibu, hadi Gonzalo Higuain alipojibu: "Sote tunajua nini kimetukuta, tunahitaji hewa. Hatuwezi kupumua hapa."

Kisha Sergio Ramos akasema: "Mchohitaji kufanya ni kukomaa zaidi. Kufanya mazoezi kama mnacheza mechi!

"Hatuwezi kumtegea mtu kama Xabi akimbie kwa ajili ya kusaidia ku-cover nafasi za watu wanne kwa mwili alionao!"

Cristiano Ronaldo hakusikika wakati wa majibizano.

Mourinho alirejea kunyamazisha majibizano.

"Sahauni hayo. Tutazungumza Jumatano baada ya mechi ya Ligi Klabu Bingwa."

No comments:

Post a Comment