Tuesday, September 11, 2012

RONALDO ALIKATALIWA KUHAMA KUFUATA MSHAHARA MNONO NDO AKASUSA REAL MADRID

Ronaldo

MSHAMBULIAJI asiye na furaha wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo alifahamishwa na rais Florentino Perez kwamba waliletewa ofa ya mshahara wa euro milioni 20 kwa mwaka kutoka katika klabu moja iliyokuwa ikimuhitaji. Kwa sasa Ronaldo analipwa euro milioni 10 kwa mwaka Real. 

Televisheni ya ABC imesema kwamba katika mkutano maarufu wa Septemba 1 uliofanyika Santiago Bernabeu, Ronaldo aliambiwa na Perez na makamu wa rais Jose Angel Sanchez kwamba klabu ambayo haitajwi iliwasilisha ofa ya ada ya uhamisho ya euro milioni 95 na kwamba iko tayari kumlipa mshahara wa euro milioni 20 kwa mwaka lakini wakakataa. 

Perez hakumtajia jina la klabu hiyo lakini ilielezwa kwamba dirisha la usajili lilikuwa bado liko wazi katika nchi za Ufaransa na Urusi, huku PSG na Anzhi zikitarajiwa kuwa bila ya shaka ndizo zilizotuma ofa hiyo ya kumchukua Ronaldo. 

Imekuja kugundulika kuwa, siku moja baada ya Ronaldo kupewa taarifa hizo na rais Perez, ndipo alipowaambia waandishi wa habari baada ya mechi yao dhidi ya Granada kwamba hana furaha Real.

No comments:

Post a Comment