Wednesday, September 19, 2012

MOURINHO ASEMA REAL WALIPAMBANA KAMA WANYAMA RONALDO AKIIZAMISHA MAN CITY, ARSENAL YAPIGA MTU KWAO

Straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Manchester City wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Manchester City wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS
Kipa wa Manchester City, Joe Hart akijilaumu baada ya straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo (hayupo pichani) kufunga goli lao la tatu wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS


Straika Karim Benzema (kushoto) akishangilia goli lake pamoja na mchezaji mwenzake Angel Di Maria baada ya kufunga goli lao la pili dhidi ya Manchester City wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Straika wa Zenit St. Petersburg, Hulk akitembea wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa dhidi ya Malaga kwenye Uwanja wa La Rosaleda mjini Malaga jana Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Straika wa Zenit St. Petersburg, Hulk (kulia) akianguka jirani na mchezaji wa Malaga, Martin Gaston Demichelis wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa kwenye Uwanja wa La Rosaleda mjini Malaga jana Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Beki ya Manchester City, Matija Nastasic (juu) akikaa juu ya straika wa Real Madrid, Karim Benzema wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Straika wa Real Madrid, Karim Benzema akigongana na beki wa Manchester City, Matija Nastasic (juu) wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Kipa wa Manchester City, Joe Hart akishindwa kuokoa shuti la beki wa Real Madrid, Marcelo wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho (katikati) akitoa maelekezo jirani na wachezaji wake Cristiano Ronaldo (kushoto) na  Karim Benzema wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Kiungo wa Manchester City, Gareth Barry (mbele) na beki Matija Nastasic wakiondoka vichwa chini mwishoni mwa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Kiungo wa Manchester City, Gareth Barry (mbele) na beki Matija Nastasic wakiondoka vichwa chini mwishoni mwa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Straika wa Paris St Germain, Zlatan Ibrahimovic akimiliki mpira wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa dhidi ya Dynamo Kiev kwenye Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris, jana Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS
 
Straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo (kushoto) akishangilia pamoja na mchezaji mwenzake Pepe baada ya kufunga goli dhidi ya Manchester City wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akishangilia na mchezaji mwenzake Marcelo (juu) baada ya kufunga goli dhidi ya Manchester City wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia goli la Cristiano Ronaldo (chini) dhidi ya Manchester City wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia goli la Cristiano Ronaldo (chini) dhidi ya Manchester City wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akishangilia na mchezaji mwenzake Marcelo (juu) baada ya kufunga goli dhidi ya Manchester City wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Kocha wa Montpellier, Rene Girard (kulia) akitoa amelekezo wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa kwenye Uwanja wa Stade de la Mosson mjini jana Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS
Mchezaji wa Montpellier, Garry Bocaly (kulia) akiwania mpira dhidi ya straika wa Arsenal, Gervinho wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa kwenye Uwanja wa Stade de la Mosson mjini jana Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Mchezaji wa Borussia Dortmund, Ivan Perisic (kushoto), Robert Lewandowski na Marcel Schmelzer (kulia) wakishangilia goli lao dhidi ya Ajax Amsterdam wakati wa mechi yao ya Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulya mjini Dortmund Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Mchezaji wa Montpellier, Benjamin Stambouli (kulia) akiwania mpira dhidi ya kiungo wa Arsenal, Abou Diaby wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa kwenye Uwanja wa Stade de la Mosson mjini jana Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS
Kiungo wa Paris St Germain, Javier Pastore (kushoto) na Nene wakishangilia goli lao la nne la timu yao wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev kwenye Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris, Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS
Beki wa Manchester City, Aleksandar Kolarov akishangilia baada ya kuifungia timu yake goli la pili dhidi ya Real Madrid wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS
Straika wa Manchester City, Edin Dzeko (kulia) akishangilia na mchezaji mwenzake Yaya Toure (kushoto) baada ya kufunga goli huku beki wa Real Madrid, Raphael Varane akipiga kelele wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS
Straika wa Manchester City, Edin Dzeko (kulia) akifunga goli dhidi ya Real Madrid wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Kiungo wa Manchester City, David Silva (kushoto) akipumzishwa na Edin Dzeko wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS
Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps (kulia), mcheza kikapu wa NBA Mfaransa Tony Parker na rafikiye wa kike Axelle wakishuhudia mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa baina ya Paris St Germain na Dynamo Kiev kwenye Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris, Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho (kulia) akikuna kichwa wakati kocha wa Manchester City, Roberto Mancini (kushoto) akizungumza na Aleksandar Kolarov (katikati) wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS
Mchezaji wa Montpellier, Anthony Mounier (kulia) akiwania mpira dhidi ya kiungo wa Arsenal, Mikel Arteta wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa kwenye Uwanja wa Stade de la Mosson mjini jana Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS


Kiungo wa Manchester City, David Silva (kulia) akimiliki mpira dhidi ya beki wa Real Madrid, Pepe wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS
Straika wa Arsenal, Gervinho (wa tatu kushoto) akifunga goli la pili la timu yake wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa dhidi ya Montpellier kwenye Uwanja wa Stade de la Mosson mjini Montpellier, Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Straika wa Arsenal, Gervinho (wa tatu kushoto) akifunga goli la pili la timu yake wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa dhidi ya Montpellier kwenye Uwanja wa Stade de la Mosson mjini Montpellier, Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS
Kiungo wa Manchester City, Samir Nasri (kulia) akijaribu kumiliki mpira dhidi ya kiungo wa Real Madrid, Xavi Alonso wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Mchezaji wa Montpellier, Jamel Saihi (kushoto) akijaribu kumdhibiti mshambuliaji wa Arsenal, Lukas Podolski wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa kwenye Uwanja wa Stade de la Mosson mjini Montpellier, Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS
Straika wa Manchester City, Carlos Tevez (mbele) akikimbia na mpira mbele ya beki wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa wakati wa mechi yao ya Kundi la D la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Mchezaji wa Montpellier, Hilton (kushoto) na Jamel Saihi wakimbana kiungo wa Arsenal, Abou Diaby wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa kwenye Uwanja wa Stade de la Mosson mjini Montpellier, Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

Mchezaji wa Montpellier, Hilton (kushoto) akiwania mpira dhidi ya straika wa Arsenal, Olivier Giroud wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa kwenye Uwanja wa Stade de la Mosson mjini Montpellier, Septemba 18, 2012. Picha: REUTERS

MADRID, Hispania
REAL Madrid walionyesha ujasiri wa upambanaji ambao ulikosekana katika mechi za karibuni kiasi cha kumfanya kocha kuhoji malengo ya wachezaji, Jose Mourinho mwenye faraja alilipuka baada ya timu yake kupambana na kuifunga Manchester City 3-2 jana usiku.

Cristiano Ronaldo alifunga goli la ushindi la dakika ya 90 na kuipa Real mwanzo mzuri wa ushindi wa Kundi D la Ligi ya Klabu Bingwa, baada ya kutaguliwa mara mbili katika mechi iliyojaa ushindani kwenye Uwanja wa Bernabeu.

"jambo la muhimu zaidi kwangu ni kujivunia timu bila ya kujali matokeo," Mourinho mwenye furaha aliuambia mkutano na waandishi wa habari, baada ya kushangilia kwa kuteleza kwa magoti huku akirushua ngumi hewani wakati akishangilia goli la ushindi la Ronaldo.

"Nimekuwa nikiwaambia jambo moja wachezaji. Tunaweza kupoteza mechi kama ya leo, sio tatizo, lakini muhimu ni kupambana kama wanyama hadi dakika ya mwisho."

Real wameanza vibaya kampeni za kutetea ubingwa wa La Liga, kwa kupata pointi nne tu kati ya 12 walizowania hadi sasa.

Kipigo chao cha karibuni cha 1-0 kutoka kwa Sevilla, kiliamsha hasira za Mourinho aliyehoji kujitolea kwa wachezaji wake jambo ambalo lilikuwa bado ni gumzo katika mji mkuu wa Hispania kuelekea mechi ya jana.

"Hatuwezi kufungwa kama tulivyofungwa na Getafe au Sevilla," alisema kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Inter Milan, ambaye alikanusha uvumi kwamba kuna mvurugano wa ndani ya kikosi.

"Leo tulikuwa na usongo zaidi, nguvu, tulitawala, na hatimaye kushinda. Tuliruhusu magoli mawili lakini tuliendelea kupambana. Tulisawazisha lakini tuliendelea kwenda.

"Mimi si kitu katika historia ya Real Madrid lakini nina haki ya kusema kwamba mashabiki wa Madrid wanataka kuona hivi. Tunaweza kucheza soka tamu, lakini ilikuwa ngumu leo.

"Hali ya kujiamini ilikuwa chini, lakini jambo muhimu ni kujitolea kwa wachezaji. Hii ni DNA ya msimu uliopita. Ni hatua muhimu katika kundi gumu."

Edin Dzeko na kisha Aleksandar Kolarov waliwafungia Man City magoli yaliyowaweka mbele kabla ya Karim Benzema na Ronaldo kufunga magoli ya dakika za lala salama kwa Real.

"Ni ngumu, sio kwa sababu tumefungwa ila kwa sababu tulikuwa tunaongoza 2-1 dhidi ya timu kama Real Madrid 2-1 zikiwa zimebaki dakika nne mechi kumalizika," kocha wa Man City, Roberto Mancini alisema.

"Ni lazima tuongeze kiwango kwa sababu tunarudi nyuma mno wakati mwingine. Tuliwaruhusu wapinzani kucheza nje ya eneo la hatari. Tulifanya kosa hili."

Mancini alikataa kukubali kisingizio cha ugeni wa michuano kwa mabingwa hao wa ligi kuu ya England ambao wanashiriki kwa mara ya pili ligi ya klabu bingwa, kuwa ndio sababu ya kupoteza ushindi katika dakika za mwisho .

"hatuwezi kuendelea kuzungumzia uzoefu. Tuna wachezaji ambao wanacheza katika kiwango cha kimataifa. Tunahitaji kujiboresha  na kufadhaishwa na matokeo haya," alisema.

"Tulifunga magoli mawili ambayo yalikuwa mazuri, makosa yetu yalikuwa ni kurudi nyuma mno."No comments:

Post a Comment