Mhe. Rais Kikwete (kulia) akiwa na Mhe. Tundu Lissu |
Mhe. Tundu Lissu (kulia) akiwa na Spika wa Bunge, Mhe. Anna Makinda. |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ni
miongoni mwa viongozi wa juu serikalini watakaoshiriki tukio la kuuaga mwili wa baba wa Mbunge wa
Singida Mashariki (CHADEMA), Mhe. Tundu Lissu, aliyefariki dunia Jumapili
kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akizungumza
leo, Mhe. Tundu Lissu amesema kuwa shughuli za kumuaga marehemu baba yake zitafanyika
kesho kuanzia asubuhi nyumbani kwake (Mhe. Tundu Lissu), eneo la Tegeta jijini
Dar es Salaam na kwamba, wamejulishwa kuwa Rais Kikwete ni miongoni mwa
viongozi watakaohudhuria.
Akieleza
zaidi, Mhe. Lissu amesema kuwa ratiba ya tukio hilo itaanza saa 5:00 asubuhi,
misa ya marehemu itaanza saa 7:00 mchana na baada ya hapo, litafuatia tukio la
kusoma wasifu na na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu kabla ya kuanza safari
ya kwenda kuzika nyumbani kwao Mahambe, katika wilaya mpya ya Ikungi mkoani
Singida.
"Mzee
amefariki akiwa na miaka 86. Tumejaribu sana kumtibu, Mungu ndiye anayejua
zaidi... tunashukuru sana kwa ushirikiano mkubwa tunaopata kutoka kwa ndugu na
jamaa," amesema Mhe. Tundu Lissu leo wakati akihojiwa na mtandgazaji Anord
Kayanda wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa jioni na kituo cha redio cha Clouds
FM.
No comments:
Post a Comment