Mjengo wenyewe nd'o huu |
Mchungaji Lwakatare akizungumza siku akiuzindua. |
Samani za ndani ya mjengo |
Kitanda ndani ya mjengo |
Mc akiwa kazini siku ya uzinduzi wa mjengo huo... hapa ni sehemu mojawapo ndani ya mjengo |
Hapa mchungaji akipozi kwa picha na Mc siku ya uzinduzi wa mjengo. |
Mc na mwenzake wakiwa kwenye kochi ndani ya mjengo huo. |
Kujisevia misosi siku ya uzinduzi wa mjengo. |
Imeelezwa kuwa salama pekee ya mjengo wa Mama Lwakatare unaokadiriwa kuwa na thamani ya Sh. bilioni 1.5 itategemea maamuzi ya mahakama ambayo hadi sasa ndiyo iliyositisha zoezi la kulivunja.
Jana, Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Manchare Heche, alikaririwa katika taarifa ya gazeti la NIPASHE akithibitisha kuwapo kesi iliyofunguliwa na mmiliki wa jumba hilo katika Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi na kwamba itatajwa wiki ijayo (Septemba 20, 2012).
Baadhi ya majumba katika maeneo hayo yameshabomolewa katika operesheni ambayo pia ilihusisha Wizara ya Maliasili na Utalii na kusimamiwa na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha Jeshi la Polisi, Julai 7, mwaka huu, lakini jumba la Mama Lwakatare liliachwa kutokana na kuwapo zuio la mahakama.
No comments:
Post a Comment