Monday, September 3, 2012

MISS KIGAMBONI WASAIDIWA FEDHA ZA MAANDALIZI

Diwani wa Kata ya Kibada, Kigamboni (CUF), Juma Nkumbi (wa tatu kutoka kushoto), akiwa na Diwani wa Vijibweni, Kigamboni (CCM), Suleiman Mathew (anayemfuatia) katika ukumbi wa City Sports Lounge asubuhi hii, wakati wa kukabidhi fedha za maandalizi kwa wawakilishi wa Miss Kigamboni, kwenye shindano la Miss Temeke 2012, linalotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu.  Wengine kulia ni warembo, Eddah Sylvester (Miss Kigamboni 2012) na Esther Albert (Miss Kigamboni namba 4). Kushoto ni Agness Goodluck (Miss Kigamboni namba 2). 

Diwani wa Kata ya Kibada, Kigamboni (CUF), Juma Nkumbi kulia, akimkabidhi fedha Mratibu wa Miss Kigamboni 2012, Somoe Ng’itu kwa ajili ya maandalizi ya wasichana wake kwenye shindano la Miss Temeke 2012. Katikati ni Diwani wa Vijibweni, Kigamboni (CCM), Suleiman Mathew, na anayemfuatia ni Agness Goodluck (Miss Kigamboni namba 2). Zoezi hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa City Sports Lounge asubuhi hii.

No comments:

Post a Comment