Chicharito wa Manchester United akipiga shuti wakati wa mechi yao ya raundi ya tatu Kombe la Capital One dhidi ya Newcastle United kwenye Uwanja wa Old Trafford jana Septemba 26, 2012. |
Chicharito wa Manchester United akipiga shuti wakati wa mechi yao ya raundi ya tatu Kombe la Capital One dhidi ya Newcastle United kwenye Uwanja wa Old Trafford jana Septemba 26, 2012. |
LONDON, England
Chelsea watawakaribisha Manchester United katika mechi yao ya Kombe la Capital One (zamani Carling Cup) baada ya klabu hizo mbili kupangwa pamoja katika ratiba ya raundi ya nne ya michuano hiyo jana.
Man U, ambaye ni mabingwa mara nne wa kombe hilo, waliwafunga Newcastle United mabao 2-1 jana na kuandaa na mazingira ya kukutana na Chelsea ambao juzi waliwasambaratisha Wolverhampton Wanderers kwa kuwapa kipigo cha mabao 6-0 katika mechi yao ya raundi ya tatu.
Kocha wa Liverpool (iliyoshinda 2-1 mechi ya kombe hilo jana dhidi ya West Brom Albion), Brendan Rodgers ataikaribisha klabu yake ya zamani ya Swansea City na wanafainali wa 2011, Arsenal watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Reading baada ya vijana wa kocha Arsene Wenger kushinda pia jana kwa mabao 6-1 dhidi ya Coventry City.
Leeds United, ambao waliwashangaza Everton kwa kuwafunga juzi, watakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Southampton huku wababe wa Manchester City, Aston Villa wakisafiri kwenda kucheza dhidi ya Swindon Town.
Mechi hizo za raundi ya nne zitaanza kuchezwa Oktoba 29.
RATIBA RAUNDI YA NNE CAPITAL CUP
Sunderland v Middlesbrough
Swindon Town v Aston Villa
Wigan Athletic v Bradford
Leeds United v Southampton
Norwich City v Tottenham Hotspur
Liverpool v Swansea City
Chelsea v Manchester United
No comments:
Post a Comment