Thursday, September 13, 2012

KAMATI YA UTENDAJI TFF YAREKEBISHA KANUNI LIGI YA WILAYA, MKOA


KAMATII ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Septemba 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam imepitisha marekebisho ya kanuni kwa ajili ya Ligi ya Mkoa na Ligi ya Wilaya.

Afisa habari wa TFF, Boniface Wambura amesema leo kuwa marekebisho hayo yametokana na mabadiliko ya mfumo wa mashindano uliofuta Ligi ya Taifa. Hivi sasa kutakuwa na Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Mkoa na Ligi ya Wilaya.

Alisema kutokana na marekebisho hayo ya kanuni; Ligi ya Wilaya itaendeshwa na Vyama vya Mpira wa Miguu vya Wilaya (DFAs), Ligi ya Mkoa itaendeshwa na Vyama vya Mpira wa Miguu vya Mikoa (RFAs).

Aliongeza kuwa mechi za mchujo (play offs) kutafuta timu zitakazopanda kwenda Ligi ya Mkoa zitaendeshwa na RFAs wakati play offs za kupanda Ligi Daraja la Kwanza zitakazohusisha mabingwa wa mikoa zitasimamiwa na TFF.

Alisema ligi za madaraja yote zitachezwa mwaka mzima kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

No comments:

Post a Comment