Thursday, September 20, 2012

JACK WILSHERE WA ARSENAL APONA... AJIFUA NA WENZAKE BAADA YA KUWA NJE YA KIKOSI MIEZI 14

Jack Wilshere
Emmanuel Frimpong
LONDON, England
Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere amerudi kikosini na kujifua na wenzake katika muda wote wa mazoezi leo baada ya kuwa nje kwa miezi 14 kutokana na jeraha la muda mrefu la 'enka'.

Kiungo huyo mwenye miaka 20 alikuwamo katika kikosi cha kwanza cha Arsenal na kuitwa pia katika kikosi cha timu ya taifa ya England kabla ya kuondolewa baadaye.

"Tumefurahi sana, Jack amerudi kamili mazoezini. Amekuwa nje kwa miezi 14 na hicho ni kipindi kirefu kwa mtu wa umri wake. Ni habari njema," kocha Arsene Wenger ameiambia tovuti ya klabu yake (www.arsenal.com).

Kiungo mwenzake Emmanuel Frimpong pia amerudi mazoezini baada ya kuumia goti Februari wakati akichezea Wolverhampton Wanderers kwa mkopo.

Wote, Wilshere na Frimpong watakabiliwa na kazi ngumu ya kurejea katika kikosi cha kwanza baada ya  Wenger kumleta kiungo wa timu ya taifa ya Hispania, Santi Cazorla na Arsenal kuanza vizuri msimu huu wa Ligi Kuu ya England, wakishika nafasi ya tatu baada ya mechi nne.

No comments:

Post a Comment