Sunday, September 30, 2012

FERGUSON AMBWATUKIA REFA KWA KUONGEZA DAKIKA NNE TU ZA MAJERUHI WAKATI MAN U WAKICHEMSHA KWA TOTTENHAM NA KUCHAPWA NYUMBANI KWAO OLD TRAFFORD KWA BAO 3-2... CHELSEA YAICHAPA ARSENAL, LIVERPOOL YAUA 5-2, MANCHESTER CITY YASHINDA 2-1

Dah... basi tena! Kocha Alex Ferguson wa Man U akiangalia saa yake wakati mechi yao dhidi ya Tottenham ikielekea kumalizika.
Shinji Kagawa wa Man U akishangilia bao alilofunga dhidi ya Tottenham.
Van Persie wa Man U akimtoka Gallas (katikati) na wenzake wa Tottenham jana.
Fernando Torres na John Terry wa Chelsea wakishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates jijini London jana.
MANCHESTER, England
Kocha wa Man U, Alex Ferguson ameelezea kutoridhishwa na dakika za majeruhi zilizoongezwa wakati timu yake ikipata kipigo cha nyumbani cha mabao 3-2 kutoka kwa Tottenham, akidai kwamba dakika nne tu zilizoongezwa katika mechi hiyo ni matusi kwa mchezo wa soka.


Man U walijikuta wakiwa nyuma kwa mabao 2-0 hadin kufikia mapumziko lakini mabao mawili kutoka kwa Nani na Shinji Kagawa yaliwapa nafuu vijana wa Ferguson katika kipindi cha pili.

Man U walitawala mechi katika sehemu kubwa ya kipindi cha pili , lakini Tottenham wakajihakikishia ushindi wao wa kwanza kwenye Uwanja wa Old Trafford baada ya miaka 23 - na Ferguson anaamini kwamba refa alipaswa kuongeza dakika nyingi zadi baada ya kumalizika kwa dakika 90 za kawaida.

"Walitupa dakika nne za nyongeza, hili ni tusi kwa mchezo wa soka.” amewaambia waandishi wa habari.

“Inakupunguzia nafasi ya kushinda mechi ya soka.

"Kulikuwa na mabadiliko ya wachezaji sita... kwahiyo hapo tayari dakika nne zimepotea na kipa ni lazima  alipoteza muda kwa dakika mbili au tatu na kila mara walichelewa kwa makusudi kuanzisha mpira kutokea golini kwao."

Licha ya kufungwa dhidi ya Tottenham, Ferguson alielezea kuvutiwa kwake na kiwango kizuri kilichoonyeshwa na timu yake katika kipindi cha pili.

CHELSEA YAICHAPA ARSENAL, BA SAFI NEWCASTLE

Katika mechi nyingine jana, Chelsea walishinda ugenini 2-1 dhidi ya Arsenal, Liverpool wakaishindilia Swansea mabao 5-2, Newcastle wakatoka sare ya 2-2 dhidi ya Reading huku Manchester City wakishinda 2-1 dhidi ya Fulham.

MECHI ZA JANA ENGLAND KWA KIFUPI:

Sunderland        1 Steven Fletcher 51                                  
Wigan Athletic    0                                                     
Kadi nyekundu: Jordi Gomez 48
Hadi Mapumziko: 0-0; Mashabiki waliohudhuria: 37,742

Reading           2 Jimmy Kebe 58, Noel Hunt 62                         
Newcastle United  2 Demba Ba 59,83                                      
Hadi Mapumziko: 0-0; Mashabiki waliohudhuria: 24,097

Everton           3 Leon Osman 25, Nikica Jelavic 32,37                 
Southampton       1 Gaston Ramirez 8                                    
Hadi Mapumziko: 3-1; Mashabiki waliohudhuria: 37,922

Fulham            1 Mladen Petric 10pen                                 
Manchester City   2 Sergio Aguero 43, Edin Dzeko 87                     
Hadi Mapumziko: 1-1; Mashabiki waliohudhuria: 25,698

Norwich City      2 Steve Morison 61, Grant Holt 87                     
Liverpool         5 Luis Suarez 2,38,57, Nuri Sahin 47, Steven Gerrard 68
Hadi Mapumziko: 0-2; Mashabiki waliohudhuria: 26,831

Stoke City        2 Peter Crouch 12,36                                  
Swansea City      0                                                     
Hadi Mapumziko: 2-0;  Mashabiki waliohudhuria: 27,330

Arsenal           1 Gervinho 42                                         
Chelsea           2 Fernando Torres 20, Juan Mata 53                    
Hadi Mapumziko: 1-1;  Mashabiki waliohudhuria: 60,101

No comments:

Post a Comment