Saturday, September 1, 2012

DILI LA MOUTINHO KWENDA SPURS KWA PAUNDI MIL.22 LAKWAMA DAKIKA YA MWISHO.... PORTO WALISHAKUBALI MZIGO, DIRISHA LIKAFUNGWA


 JARIBIO la Tottenham la kutaka kumsajili kiungo wa Porto, Joao Moutinho. limekwama katika siku ya mwisho ya usajili.

Spurs walitoa ofa paundi milioni 22, ambayo ingeweka rekodi ya klabu hiyo, ambayo ilikubaliwa na Porto kwa ajili ya nyota huyo wa timu ya taifa ya Ureno mwenye umri wa miaka 25 jana Ijumaa lakini klabu hiyo ya London kaskazini ilishindwa kukamilisha dili hilo na mawakala wake wakati dirisha lilipofungwa saa 5.00 usiku wakiwa bado katika mabishano ya malipo binafsi ya mchezaji.

Moutinho alichukuliwa kama mrithi sahihi wa Luka Modric katika dimba la kati la Tottenham baada ya kiungo huyo wa Croatia kujiunga na Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 33.2 mapema wiki hii.

Rafael van der Vaart akafuata njia ya mchezaji huyo wa zamani Dinamo Zagreb ya kutokea White Hart Lane jana Ijumaa, akijiunga na Hamburg kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 10.3, na kuongeza hitaji la Spurs la kiungo.

Spurs waliimarisha kiungo chao kwa kumsajili Mousa Dembele Jumatano, lakini Moutinho atabaki katika klabu yake ya Porto licha ya mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy kujaribu kusukuma mambo yaende haraka katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili.


No comments:

Post a Comment