Thursday, August 23, 2012

ZIDANE NI ZAIDI YA MESSI NA RONALDO - CAZORLA

Zinedine Zidane akifunga bao la ushindi wa Ligi Klabu Bingwa kwa Real Madrid wakati wa mechi yao ya fainali dhidi ya Bayer Leverkusen mwaka 2002. Goli hilo litabaki kuwa moja ya mabao bora kabisa kufungwa katika historia ya soka.
Zinedine Zidane (kushoto) akiwa na mkewe Veronique Zidane mjini Geneva, Uswisi Januari 17, 2012.
Lionel Messi wa Barcelona akichungwa na msitu wa wachezaji wa Arsenal

 Lionel Messi (wa tatu kulia) wa Barcelona akifunga goli kutokea katikati ya msitu wa wachezaji wa Arsenal wakati wa mechi yao ya marudiano ya robo fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona Aprili 6, 2010. Picha: REUTERS
Messi akiwekwa mtu kati na wachezaji wa Real Madrid
Messi akiwekwa mtu kati na wachezaji wa Man United
Lassana hadi kasmshika mkono... huendi kokote
Messi akichungwa na wachezaji wa Man United
Ronaldo akishangilia baada ya kutupia... ndio zake
Ronaldo akishangilia baada ya kutupia...

Chezea mimi wewe...?

NYOTA wa Arsenal, Santi Cazorla amesema gwiji wa Ufaransa Zinedine Zidane ni mwanasoka bora kuliko wote aliopata kukabiliana nao kushinda straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo au Lionel Messi wa Barcelona.

Kiungo huyo wa zamani wa Villarreal na Malaga alikabiliana na Zizzou mara kadhaa wakati akichechezea Madrid, na Mfaransa huyo ndiye aliyemvutia zaidi Cazorla.

"Katika kipindi cha maisha yako daima unakuwa na wachezaji tofauti unaowapenda. Nilipokuwa mtoto, kwa sababu baba yangu aliipenda 'Dream Team', nami nilimpenda Michael Laudrup," mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Hisoania alisema.

"Lakini daima nimekuwa nikisema mchezaji bora miongoni mwa niliopata kukabiliana nao, na mchezaji aliyekuwa fundi zaidi, alikuwa ni Zidane. Kuna Messi na Ronaldo, lakini bado nadhani kupata bahati ya kucheza dhidi ya Zidane, na kumshuhudia akicheza, alikuwa ni wa kipekee. Yeye bado ni bora.

"Aliokuwa akionekana kama mchezaji wa vurugu kutokana na urefu wake, lakini baadaye unabaini kwamba alikuwa 'fundi' sana na aliyejaliwa kipaji awapo na mpira. Nili-injoi sana kumwangalia akicheza, ilikuwa ni raha sana. Naweza kubainisha kila kitu kuhusu yeye, kwa sababu alikuwa na kila kitu kinachohitajika ili kuwa mchezaji bora."

Zidane alivaa jezi za Cannes, Bordeaux, Juventus na Real Madrid katika kipindi chake cha kucheza soka, na pia aliichezea timu yake ya taifa zaidi ya mechi 100 na alitwaa Kombe la Dunia na Ulaya.

No comments:

Post a Comment