Friday, August 24, 2012

YANGA YAUA RAYON 2-0 KIGALI

Wachezaji wa Yanga wakipasha nchini Rwanda. PICHA: SALEH ALLY WA CHAMPIONI

MABINGWA wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) wameanza kwa kishindo ziara yao ya nchini Rwanda kwa ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Rayon Sport katika mechi yao ya kirafiki kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali leo jioni.

Yanga ilipata goli la kwanza mapema katika dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa Mganda Hamis Kiiza 'Diego' na wakaongeza la pili katika dakika ya 12 lililofungwa na yosso wao Simon Msuva. 

Timu hiyo ilipata nguvu nchini humo baada ya kuungana na beki wao mpya Mbuyu Twite waliyemsajili baada ya kuwapiku mahasimu wao Simba.

Yanga iko Kigali kutokana na mwaliko wa Rais Paul Kagame na itakaporejea nchini wiki ijayo itaitikia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika Ikulu ya nchini jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment