Friday, August 17, 2012

VAN PERSIE ANALETA MSIMU WA "MVUA" ZA MAGOLI - WELBECK

Danny Welbeck
Robin Van Persie (katikati) akishangilia goli lake la pili dhidi ya Sunderland pamoja na Theo Walcott (kushoto) wa Arsenal wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London Oktoba 16, 2011. Picha: REUTERS
Robin Van Persie (kulia) akishangilia goli lake la pili dhidi ya Sunderland pamoja na Theo Walcott (kushoto) wa Arsenal wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London Oktoba 16, 2011. Picha: REUTERS

Robin Van Persie (chini) akishangilia goli lake dhidi ya Sunderland pamoja na Theo Walcott wa Arsenal wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London Oktoba 16, 2011. Picha: REUTERS

Robin Van Persie akishangilia goli lake la pili dhidi ya Sunderland England kwenye Uwanja wa Emirates mjini London Oktoba 16, 2011. Picha: REUTERS

Gervinho wa Arsenal (kushoto) akishangilia pamoja na Robin Van Persie baada ya kumpikia goli kwa krosi wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Stoke City kwenye Uwanja wa Emirates London Kaskazini Oktoba 23, 2011. Picha: REUTERS

DANNY Welbeck amebashiri kwamba msimu huu Manchester United itanyeshea wapinzani wao "mvua za magoli".

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya England huenda akapoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza kutokana na kuwasili kwa mshambuliaji anayefunga mabao bila ya "breki" Robin van Persie aliyesajiliwa kwa paundi milioni 22 kutoka Arsenal.

Lakini alisema: "Robin ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa sana na nimshambuliaji wa kiwango cha dunia.

"Anaweza kufuga magoli na kupikia wenzake nafasi za kufunga. Wao ni aina ya wachezaji wanayokusaidia kutwaa mataji.

"Ni bonge la usajili kwa klabu yetu, kila mmoja amefurahi. Ninajiandaa kucheza pamoja naye."

Welbeck (21) aliongeza: "Hapa Man United unajifunza kucheza na aina tofauti za washambuliaji na wachezaji.

"Tutakapoanza kufanya mazoezi pamoja nadhani kila mtu tunatengeneza ushirikiano baab'kubwa — itakuwa ni mvua za magoli tu kwa Manchester United."

No comments:

Post a Comment