Monday, August 6, 2012

SHIBUDA AICHURIA NAFASI YA NAPE NNAUYE CCM

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye
Mhe. John Shibuda
Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi, John Magale Shibuda (CHADEMA) ametoa kali ya jioni hii bungeni mjini Dodoma baada ya kutaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimpe Waziri Benard Membe cheo cha kuwa katibu wa Itikadi na Uenezi kwa madai kuwa ni mchapakazi hodari na pia ana sifa zote za kushika wadhifa huo.

Mhe. Shibuda ameyasema hayo wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inayoongozwa na Waziri Membe; hatua ambayo kama kweli ikitekelezwa kivitendo na CCM, itamaanisha kuwa Nape Nnauye atapoteza cheo anachokishikilia sasa -- cha kuwa Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Katika hatua nyingine, Shibuda alimtaka Waziri Membe ajitahidi kuiacha wazi simu yake kwa muda mwingi kutokana na kile alichodai kwamba imekuwa haipatikani kwa asilimia 95, jambo ambalo alisema si jema kwavile anapaswa kupatikana kirahisi ili asaidie kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi; huku akihoji kuwa kama yeye aliye swahiba wake mkubwa anampata kwa shida kupitia simu yake hiyo; "hali itakuwaje kwa wananchi wengine."No comments:

Post a Comment