Wednesday, August 29, 2012

DEMBELE ATUA SPURS BAADA YA KUFUZU VIPIMO

Moussa Dembele

TOTTENHAM Hotspur wameafiki kumsajili kiungo mchezesha timu wa Ubelgiji Moussa Dembele kutoka Fulham, klabu hizo za Ligi Kuu ya England zimetangaza leo jioni.

Dembele amecheza mechi 74 akiwa na Fulham na amefunga magoli saba baada ya kujiunga na klabu hiyo ya London akitokea katika klabu ya Uholanzi ya AZ Alkmaar mwaka 2010.

"(Dembele) amefuzu vyema vipimo vya afya na atasaini (kujiunga na Tottenham) kwa ada ya uhamisho ambayo haitajwi," taarifa katika tovuti ya Fulham (www.fulhamfc.co.uk) imesema.

No comments:

Post a Comment