Tuesday, August 7, 2012

REDONDO: SINA MKATABA NA AZAM


KIUNGO Ramadhani Chombo 'Redondo' amesema leo kwamba yeye ni mchezaji halali wa Simba baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa dau la Sh. milioni 30 akitokea Azam.

Akizungumza katika ofisi za Shirikisho la Soka nchini (TFF), Redondo amesema hakuna sababu ya kuwapo kwa mjadala kuhusu uhamisho wake kwa kuwa hauna utata wowote.

Amesema mkataba wake na Azam ulimalizika Juni mwaka huu na kwamba hivi sasa yuko huru kuichezea Simba, ambayo imempatia alichotaka.

Redondo, nyota mwingine aliyetua kutoka Azam, Mrisho Ngassa, beki Mbuyu Twite kutoka APR na Emmanuel Okwi, ambaye alikwenda kujaribu kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa Austria, ni kati nyota wa Simba watakaotambulishwa kesho kwenye Tamasha la Simba Day litakalofanyika kuanzia saa 4 asubuhi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo litahitimishwa na mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya wenyeji Simba dhidi ya Nairobi City Stars ya Kenya huku Maveterani wa Simba wa Tabata wakiwakaribisha watani zao katika mchezo mwingine utakaofanyika  kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tabata.

No comments:

Post a Comment