Friday, August 31, 2012

REDD'S MISS MWANZA, KANDA YA MASHARIKI NI MOTO

Warembo wa Jiji la Mwanza wanaotaraji kupanda jukwaani leo Ijumaa Agosti 30, 2012 katika ukumbi wa Yatch Club kuwania taji la REDD'S MISS MWANZA 2012 wakiwa katika pozi mbalimbali. Shindano hilo linataraji kuwakutanisha miamba wawili wa miondoko ya pwani, Bibie Hadija Omar Kopa na mkongwe Mwanahawa Ali na mkali mwingine wa mduara, Bob Haisa.

Na Mwandishi Wetu
SAFARI ya kuwania taji la Redd’s Miss Tanzania inaendelea kushika kasi, wakati leo kutakapokuwa na shindano la kumsaka Redd’s Miss Mwanza, huku kesho Redd’s Miss East Zone akipatikana Morogoro.

Shindano la Redd’s Miss Mwanza linatarajiwa kufanyika Yacht Club kuanzia saa 2 usiku na kushirikisha warembo wapatao 16, ambao wanataka kulitwaa taji hilo kutoka kwa Irene Karubaga.

Irene ndiye Redds Miss Mwanza mpaka sasa na kunatarajiwa kuwa na burudani kibao kutoka kwa Khadija Kopa, Mwanahawa Ally pamoja na wasanii wengine.

Mratibu wa shindano hilo, Peter Omari alisema kila kitu kimekamilika na kiingilia kinatarajiwa kuwa Sh 50,000 kwa viti maalumu na vilivyobaki ni Sh 20,000.

Muandaaji wa shindano la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki, Alexander Nikitas alisema mchuano huo utakaoshirikisha warembo 12 utafanyika katika Ukumbi wa hoteli ya Nashera.

Warembo kutoka Mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara na pwani ndio wanaotarajiwa kuliwania taji hilo ambalo linashikiliwa na  Loveness Flavia.

Kiingilio kitakuwa Sh 20,000 kwa viti maalum na Sh 5,000 huku msanii Wanne Star na wengine kibao wa Morogoro wakishiriki kutoa burudani.

Shindano la Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original, ambacho kinazalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

No comments:

Post a Comment