Tuesday, August 28, 2012

ONA JINSI LUKA MODRIC ALIVYOJIFUA KWA MARA YA KWANZA NA WACHEZAJI WENZAKE REAL MADRID KUJIANDAA KWA MECHI DHIDI YA BARCELONA

Jembe Luka Modric akijifua na wachezaji wenzake wa Real Madrid leo. 
Luka Modric (kushoto) akiendelea kujifua na wenzake leo.
Sijui nitapata namba kesho niwaonyeshe kazi Barcelona? Luka Modric akijifua na wachezaji wenzake wa klabu yake mpya ya Real Madrid huku akifuatiliwa kwa karibu na kocha Jose Mourinho.   
Luka Modric (kulia, nyuma)... hapa akiendelea kujifua na wachezaji wenzake wa Real Madrid ambao ni pamoja na akina Karim Benzema, Sami Khedira na Kaka wakati wakijaindaa kwa mechi yao ya kesho kuwania taji la Super Cup dhidi ya Barcelona.
Twende sasa... Luka Modric (wa tatu kushoto mbele) akijifua na wachezaji wenzake wa Real Madrid leo. 
Haya, hebu kimbia nikuone kama uko fiti kucheza dhidi ya Barca kesho...kocha Jose Mourinho akimtazama Luka Modric wakati akijifua na wenzake wa kikosi cha Real Madrid kwa mara ya kwanza leo. 
Wenzio huwa tunafanya hivi... Luka Modric (kushoto mbele) akiongozana na Pepe (kulia) na wachezaji wengine kuendelea kujifua leo.
Safiii.... hapa kweli nimepata jembe. Kocha Mourinho akipiga makofi wakati akiiongoza timu yake katika mazoezi yao leo kujiandaa na mechi dhidi ya Barcelona kuwania taji la Super Cup kesho.
Kiungo Luka Modric amefanya mazoezi kamili leo na wachezaji wenzake wa kikosi cha Real Madrid kujiandaa na mechi yao ya marudiano ya kuwania taji la Super Cup dhidi ya Barcelona itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu kuanzia saa 5:30 usiku.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Croatia aliyekamilisha uhamisho wake jana akitokea Tottenham, alikuwa ni miongoni mwa wachezaji walioongezeka katika mazoezi ya Real Madrid leo, wengine wakiwa ni Pepe ambaye kabla ya leo alikuwa akifanya mazoezi peke yake baada ya kupona jeraha la kichwa, na pia yosso Alex na Nacho walijumuishwa.

Mourinho aliwagawa wachezaji katika makundi matatu kujiandaa na mechi ya kesho dhidi ya Barca. Katika kundi la kwanza kulikuwa na wachezaji 10 walioanza katika mechi waliyofungwa 2-1 dhidi ya Getafe juzi ambao ni Marcelo, Albiol, Arbeloa, Ramos, Lass, Xabi Alonso, Di María, Özil, Ronaldo na Higuaín. Hawa walifanya mazoezi mepesi wakiwa na kocha msaidizi, Rui Faria.

Kundi la pili lilifanya mazoezi makali zaidi na wachezaji wote waliobaki walisimamiwa na José Mourinho. Katika kundi hilo la tatu, walikuwamo Modric na wengine wakiwa ni Pepe, Álex na Nacho. Makipa Casillas, Adán na Jesús walifanya mazoezi kivyao wakiwa na kocha wa makipa, Silvino Louro.

No comments:

Post a Comment