Friday, August 24, 2012

NURI SAHIN APIMWA AFYA ARSENAL, LAKINI LIVERPOOL WATEMBEZA MKWANJA MREFU NA KUMPORA LEO AKITOKEA REAL MADRID HUKU ARSENE WENGER AKIKUBALI YAISHE LEO...!

Nuri Sahin

LONDON, England
Kocha Arsene Wenger wa Arsenal amekubali yaishe katika vita yae ya kumuwania kwa mkopo kiungo Nuri Sahin wa Real Madrid na sasa amemuachia ajiunge katika klabu ya Liverpool iliyomwaga mapesa mengi licha ya kwamba tayari nyota huyo wa kimataifa wa Uturuki alishafuzu vipimo vya afya katika klabu ya Wenger.

Gazeti la Daily Mail limesema leo kuwa Sahin anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa mkopo wa muda mrefu kuichezea Liverpool baadaye leo kufuatia Arsenal kuinuia mikono na kujiondoa katika mbio za kumtwaa kiungo huyo mwenye miaka 23.

Imeelezwa kuwa licha ya Arsenal kukaribia kumtwaa Sahin, lakini dau jipya la Liverpool lililoambatana na ofa ya kusaidia kulipa asilimia 70 ya mshahara anoendelea kulipwa na klabu yake ya Real Madrid wa paundi za England 120,000 kwa wiki ndivyo vilivyomkimbiza Wenger.

No comments:

Post a Comment