Friday, August 24, 2012

MOURINHO HAKOSI VISINGIZIO... ASEMA MSHIKA KIBENDERA ND'O KATIBUA MIPANGO YA REAL MADRID KWA KULIRUHUSU GOLI LA "OFF-SIDE" LA BARCAELONA LILILOFUNGWA NA PEDRO

Goooooohhhh....! Pedro (kushoto) akishangilia baada ya uifungia Barcelona goli la kusawazisha katika mechi yao ya kwanza ya kuwania Supercopa dhidi ya Real Madrid kwenye Uwanja wa Nou Camp jana. Barca ilishinda 3-2.
  Aaaahh... mambo gani sasa? Mbona mshika kibendera hainui kibendera kuashiria 'off-side'?  Mourinho akiwa pembeni ya uwanja wakati timu yake ya Real Madrid ikicheza ugenini dhidi ya Barcelona katika mechi yao ya kwanza ya kuwania taji la Supercopa kwenye Uwanja wa Nou Camp jana.  
Safi mwana...! Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga goli la utangulizi dhidi ya Barcelona katika mechi yao ya kuwania taji la Supercopa kwenye Uwanja wa Nou Camp jana.
Kama zali...! Di Maria (kushoto) wa Real Madrid akishangilia baada ya kufunga goli la pili dhidi ya Barcelona lililotokana na makosa ya kipa Victor Valdes aliyebaki kujiinamia wakati wa mechi yao ya Supercopa kwenye Uwanja wa Nou Camp jana.
Ronaldo akishangilia goli alilofunga jana
Yaliyopita si ndwele... leo sikutovugi tena jichoni...! Mourinho (kushoto) akisalimiana na kocha wa Barca, Tito Vilanova kabla ya kuanza kwa mechi yao ya kuwania taji la Super Cup kwenye Uwanja wa Nou Camp jana. Msimu uliopita, Mourinho alimtovuga jichoni Vilanova wakati wa mechi kama ya jana ya kuwania Supercopa kwenye Uwanja wa Nou Camp.
hawa hawaniwezi kabisaaaa....! 'Jini' Messi akiandaa mipango ya goli wakati timu yake ya Barca ikicheza dhidi mechi ya kwanza ya kuwania taji la Supercopa dhidi ya Real Madrid jana. 
Duh... ulinzi wote huu? Cristiano Ronaldo (kushoto), Fabio Coentrao (namba 5) na Xabi Alonso (kulia) wa Real Madrid wakijaribu kumzuia Lionel Messi wa Barcelona wakati wa mechi yao ya 'el clasico' kuwania taji la supercopa kwenye Uwanja wa Nou Camp jana.
Messi wa Barca (kulia) akijiandaa kupiga penati katika mechi yao dhidi ya Real Madrid jana.

Natisha kama njaaa.... Messi akishangilia goli lake alilofunga kwa penati wakati timu yake ya Barca ikicheza dhidi ya Real Madrid kuwania Supercopa kwenye Uwanja wa Nou Camp jana. 

Kwishneeee....Xavi akishangilia goli la tatu alilofunga wakati timu yake ya Barcelona ikicheza dhidi ya Real Madrid kuwania taji la Supercopa kwenye Uwanja wa Nou Camp jana. 
BARCELONA. Hispania
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho anaamini kwamba mshika kibendera alifanya “makosa makubwa” kwa kuruhusu bao la Pedro wakati timu yake ikipokea kipigo cha ugenini cha mabao 3-2 kutoka kwa Barcelona katika mechi yao ya kwanza ya kuwania taji la Supercopa la Hispania jana usiku.

Straika huyo wa timu ya taifa ya Hispania alifunga goli la kusawazisha la Barca katika dakika ya 56 baada ya kukimbia mbele ya Fabio Coentrao, lakini marejeo ya picha za video yalionyesha kwamba alikuwa ameotea (0ff-side) kabla ya kwenda kufunga goli hilo.



Real ndio waliotangulia kupata goli la kwanza kupitia kwa starika Cristiano Ronaldo aliyeunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Mesut Ozil katika kipindi cha pili kabla Pedro hajasawazisha katika dakika iliyofuata. Mabao mengine ya Barca yalifungwa kutokana na penati ya Messi iliyotolewa na Refa baada ya Sergio Ramos kumkwatua Iniesta katika eneo la 18 na jingine likawekwa wavuni na Xavi baada ya kai nzuri iliyofanywa na Iniesta.
  
“Goli la kwanza la Barcelona lilitokana na na kosa kubwa la mshika kibendera, na hivyo ndivyo ilivyokua,” alikiri Mourinho mbele ya waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mechi hiyo.

Kocha huyo Mreno pia alizungumzia kiwango cha timu yake, huku pia akimwagia sifa winga Jose Callejon.

“Sikupenda tulivyocheza kipindi cha kwanza, lakini katika kipindi cha pili, mechi ilibadilika. Callejon alicheza vizuri. Aliandaa mazingira kwa Di Maria. Hii ilikuwa mechi muhimu na nilipenda namna alivyocheza,”

Mechi ya marudiano ya Supercopa itachezwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu katika siku tano zijazo, lakini timu zote zitakuwa uwanjani kucheza mechi zao za La Liga, Ligi Kuu ya Hispania keshokutwa Jumapili, Real Madrid wakikabiliwa na mechi dhidi ya Getafe na Barcelona wakiwavaa Osasuna

No comments:

Post a Comment