Tuesday, August 7, 2012

NEYMAR: HAKUNA KAMA MESSI DUNIANI

Lionel Messi (kushoto) wa Barcelona ya Hispania na Neymar wa Santos ya Brazil wakipeana mikono baada ya mechi yao ya fainali ya Kombe la Dunia la Klabu mjini Yokohama, kusini mwa Tokyo Desemba 18, 2011. Picha: REUTERS
Lionel Messi (kulia) wa Barcelona ya Hispania na Neymar wa Santos ya Brazil wakiwania mpira wakati wa mechi yao ya fainali ya Kombe la Dunia la Klabu mjini Yokohama, kusini mwa Tokyo Desemba 18, 2011. Picha: REUTERS


NYOTA wa Santos, Neymar kwa mara nyingine amezungumzia jinsi anavyomkubali mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi, na amesema angependa kucheza naye katika kikosi kimoja siku zijazo.

"Messi hana mpinzani, ndiye bora zaidi duniani," alisema Neymar. 

"Bado nina safari ndefu sana ya kwenda kufikia kiwango chake. Nahitaji kuboresha uwezo wangu wa kufunga na ninapokuwa nimebaki uso kwa uso na kipa."

No comments:

Post a Comment