Mshindi wa Trinidad & Tobago wa medali ya dhahabu ya Olimpiki ya kurusha tufe, Keshorn Walcott (katikati) akikaribishwa na mshindi wa medali ya dhahabu wa mwaka 1976 wa Trinidad & Tobago, mwanariadha Hasely Crawford, baada ya Walcott kuwasili nchini humo akitokea kwenye Michezo ya Olimpiki ya London 2012 jana Agosti 13, 2012. Kwa kuiletea heshima nchi yake, Walcott amezawadiwa nyumba yenye thamani ya Dola za Trinidad & Tobago milioni 2.5 (sawa na Sh. milioni 606 za Tanzania), kiwanja chenye ukubwa wa futi za mraba 20,000, fedha taslimu Dola za Trinidad & Tobago milioni 1 (sawa na Sh. milioni 243 za Tanzania), na eneo la kitaifa limepewa jina lake kwenye mji aliozaliwa wa Toco ulioko pwani ya kaskazini mashariki mwa Trinidad, vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti. Picha: REUTERS |
No comments:
Post a Comment