Wednesday, August 29, 2012

MCHEZAJI AOMBEWA ITC UJERUMANI

CHAMA cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DFB) kimetuma maombi ya kupatiwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Robert Makanja ili aweze kucheza mpira wa miguu nchini humo.

DFB imetuma maombi hayo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kumwezesha mchezaji huyo kuichezea timu ya TUS Ahausen, Hessischer FuBall-Verband ambayo hata hivyo haikuelezwa iko ligi ya daraja gani nchini humo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mashindano wa DFB, Markus Stenger, Mtanzania huyo ameombewa hati hiyo kama mchezaji wa ridhaa kwa maelezo kuwa hakuwahi kusajiliwa na klabu yoyote nchini.

TFF inafanyia kazi maombi hayo na hati hiyo itatolewa mara baada ya taratibu husika kukamilika ikiwemo kubaini kama kweli mchezaji huyo hakuwahi kusajili na klabu yoyote hapa nchini.
 

No comments:

Post a Comment