Wednesday, August 8, 2012

MARIO GOMEZ NJE WIKI SITA BAADA YA KUPASULIWA ENKA

Mario Gomez
MUNICH, Ujerumani
STRAIKA wa Bayern Munich, Mario Gomez amesema kuwa amefurahishwa na upasuaji aliofanyiwa wa kifundo cha mguu, na anatarajia kurudi uwanjani mapema kadri itakavyowezekana.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani aliumia wakati Bayern wakishiriki mashindano ya LIGA Total! Cup mwishoni mwa wiki, na atakuwa nje kwa jumla ya wiki sita.

"Nimefurahi kwamba upasuaji ulienda vizuri na sasa sijisikii tena maumivu," Gomez amekaririwa akisema kupitia tovuti rasmi ya klabu yake.
"Sasa ninatakiwa kuwa mvumilivu kidogo, lakini baada ya hapo nitafanya kila nitakaloweza ili niwe tayari kupangwa tena haraka kadri itakavyozekana."

Daktari wa Bayern, Hans-Wilhelm Muller-Wohlfahrt ameeleza kwamba straika huyo nyota atapumzika kwa wiki tatu kabla ya kuanza kujifua peke yake.

"Upasuaji umeenda vizuri sana," amesema Muller-Wohlfahrt.
"Katika namna yoyote ile, Mario atapaswa kuwa nje kwa wiki tatu. Baada ya hapo, ataanza ratiba ya mazoezi mepesi."

Gomez anatarajiwa kurithiwa na Mario Mandzukic au Claudio Pizarro wakati atakapoendelea kuwa nje.
-----

No comments:

Post a Comment