Wednesday, August 15, 2012

MAJEMBE MAPYA SIMBA YASAINI MIAKA MIWILI-MIWILI, "MUZIKI" MSIMBAZI SASA UMEKAMILIKA

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hanspope (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange 'Kaburu' (katikati) wakimtambulisha beki wa kati Pascal Ochieng jijini Dar es Salaam leo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hanspope (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange 'Kaburu' (katikati) wakimtambulisha mshambuliaji Daniel Akuffo jijini Dar es Salaam leo.

WACHEZAJI wapya waliosajiliwa na Simba, beki wa kati wa timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars), Pascal Ochieng, na mshambuliaji Daniel Akuffo kutoka Hearts of Oak ya Ghana, leo wamesaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja.

Simba imewasaini wachezaji hao wapya baada ya kuwatupia virago wachezaji kadhaa iliyowasajili kabla ya michuano ya Kombe la Kagame.

Kufuatia matokeo mabaya katika Kombe la Kagame, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Bara, wamejiimarisha hivi sasa baada ya kuwasajili Mrisho Ngassa na Ramadhani Chombo 'Redondo' kutoka Azam FC pamoja na kurejea kwa nyota aliyejaribu kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Austria, Emmanuel Okwi.

Ochieng anatarajiwa kuziba pengo la Kelvin Yondani aliyetua Yanga na atashirikiana na Juma Nyosso katika eneo la ulinzi wa kati.

Uwapo kikosini wa kiungo "fundi" kama Haruna Moshi 'Boban', Mwinyi Kazimoto na beki wa "kiraka" Shomary Kapombe, "muziki" wa Simba sasa unaonekana umekamilika.

No comments:

Post a Comment