Lionel Messi |
Cristiano Ronaldo |
Andres Iniesta |
MADRID, Hispania
STRAIKA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na wachezaji wa
Barcelona, Lionel Messi na Andres Iniesta wamechaguliwa leo kuingia ‘top 3’ ya kuwania
tuzo ya UEFA ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Ulaya.
Watatu hao walipata pointi nyingi zaidi katika kura
zilizopigwa na waandishi wa habari za michezo 53 ambao waliwakilisha vyama vya
soka vya kila nchi yenye uanachama wa Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA).
Kiungo mchezeshaji wa Juventus, Andrea Pirlo alikamata
nafasi ya nne katika uchaguzi huo, huku kiungo Xavi wa Barcelona, ambaye mwaka
jana alikamata nafasi ya pili katika tuzo hiyo, alikamilisha idadi ya 'top 5'
kwa kushika nafasi ya tano.
Watatu waliobaki katika mchujo sasa watapigiwa
kura Agosti 30 kuamua mshindi wa tuzo
hiyo mjini Monaco wakati wa upangaji wa ratiba ya hatua ya makundi ya Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya.
Tuzo huyo binafsi, ilianzishwa kwa ushirikiano wa Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo wa Ulaya(ESM), lengo likiwa ni kumtunuku
mwanasoka bora, bila kujali utaifa wake, alimradi awe akiichezea klabu iliyo
katika nchi yenye uanchama wa UEFA wakati wa msimu uliotangulia.
Messi alikuwa wa kwanza kutwaa tuzo hiyo iliyoanza kutolewa mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment