Sunday, August 26, 2012

KOCHA BARCELONA ASEMA PIGA UA, ALEX SONG LAZIMA ACHEZE LEO KATIKA MECHI YAO YA LA LIGA DHIDI YA OSASUNA ITAKAYOANZA SAA 2:00 USIKU KWA SAA ZA KIBONGO...REAL MADRID VS GETAFE KUANZA 4:00 USIKU

Alex Song (kushoto) akipiga makofi wakati wa utambulisho rasmi wa kikosi cha Barca cha msimu wa 2012-13.. wengine ni Cesc Fabregas (katikati) na Jordi Alba.
Kocha wa Barcelona, Tito Vilanova amemjumuisha Alex Song katika kikosi cha timu yake kitakachocheza ugenini leo katika mechi yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Osasuna itakayoanza saa 2:00 usiku.

Song alijiunga na Barcelona wiki iliyopita akitokea Arsenal, lakini Vilanova amesema kuwa kiungo wake huyo wa kimataifa kutoka Cameroon ameonyesha kiwango cha juu mazoezini na hivyo anastahili kuwemo katika kikosi chake cha leo.

"Amekuwa na siku chache sana za kufanya mazoezi na sisi, lakini tulikuwa na muda wa kutosha kumuonyesha aina mbalimbali za uchezaji wetu... atacheza katika nafasi ya beki wa kati (Na.5) au kiungo (mkabaji)," amesema Vilanova.

"Ameonyesha kiwango kizuri sana mazoezini-- anatoka katika klabu inayofanya mazoezi yanayofanana na yetu na kujaribu kukaa na mpira," ameongeza Vilanova.

Song alitua Barca kwa ada ya uhamisho ya paundi za England milioni 15 (Sh. bilioni 37)

No comments:

Post a Comment