Friday, August 3, 2012

DARK MASTER AIBUKA NA MOJA MOJA

Rapa wa Chamber Squad, Dark Master

RAPA nyota wa kundi la Chamber Squad, Dark Master, ameachia 'ngoma' mpya ya hip hop inayokwenda kwa jina la 'Moja Moja' ikiwa katika 'audio' na video.

Dark Master ameiambia STRAIKA kuwa wimbo huo umemshirikisha nyota wa ragga nchini mshindi wa tuzo ya Kili, Hardmad.

"Wimbo umefanyika Mwanza katika studio ya One Love FX chini ya prodyuza TIDDY.

"Video imefanywa na One Love FX pia kwa sababu pale kuna studio ya muziki na kampuni ya video," alisema rapa huyo aliyepata umaarufu mkubwa aliporap katika wimbo wa kushirikishwa wa Mwana-Chamber mwenzake, Albert Mwangwair wa "She Got A Gwan".

"Ni video kali ambayo imeongozwa na Hyper na Shaibu na tayari nimeanza kuisambaza katika vituo vya TV," aliongeza.

Dark Master siku hizi ameweka maskani yake jijini Mwanza, ambako amesema anafanya kilimo na ufugaji huku akiendelea na muziki katika lebo ya One Love FX ambapo wanafanya kazi kama familia.

No comments:

Post a Comment