Ambwene Yessayah "AY" |
Shungu Ekumani a.k.a Papa Wemba |
2Face Idibia |
WANAMUZIKI maarufu barani Afrika Papa Wemba wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, 2 Face Idibia wa Nigeria, Ambwene Yessaya wa Tanzania na Daddy Owen wa Kenya watatumbuiza wakati wa fainali ya michuano ya soka ya vijana ya Airtel Rising Stars kwa nchi za Afrika zitakazofanyika kesho kwenye Uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waandaaji wa michuano hiyo, wanamuziki hao wataanza kutoa burudani kuanzia mchana ambapo kila msanii atatumbuiza kwa nyimbo zake maarufu zilizompatia umaarufu ndani na nje ya nchi yake. Baadhi ya nyimbo hizo ni ‘African Queen’, na ‘If Love Is A Crime’ za 2 Face, ‘Show Me The Way’ za Papa Wemba na ‘Bed n Breakfast‘, ‘Goodlook’ na ‘Freeze’ za AY.
Michuano hiyo iliyofunguliwa Jumatatu iliyopita na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga imeshirikisha jumla ya timu 15 za Afrika ambapo mechi yake ya fainali itaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Super Sports cha Afrika Kusini.
Nchi zilizoshiriki ni wenyeji Kenya, Tanzania, Madagascar, Malawi, Ghana, Zambia, Gabon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burkina Fasso, Chad, Congo Brazaville, Uganda, Niger, Nigeria na Sierra Leone.
Katika hatua nyingine, habari zilizotufikia kutoka Nairobi kabla ya kurusha habari hii ni kwamba timu ya Tanzania ilikuwa nyuma kwa magoli 2-1 dhidi ya Zambia katika mchezo wa mwisho uliokuwa ukichezwa kwenye uwanja Nyayo. Kama matakeo yatabaki hivyo, hio inaamanisha vijana wa Tanzania watakuwa wameaga mashindano hayo kwani mechi ya kwanza walila 1-0 mbele ya Gabon kabla ya kutoka sare ya 1-1 na Burkina Fasso.
No comments:
Post a Comment