Monday, August 27, 2012

ARSENAL BILA RVP HAIWEZEKANI, MAN CITY YAPONEA TUNDU LA SINDANO KWA LIVERPOOL

Straika wa Manchester City, Carlos Tevez akishangilia baada ya kufunga goli wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, kaskazini mwa England, Agosti 26, 2012. Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 2-2. Picha: REUTERS
Beki wa Liverpool, Martin Skrtel (kushoto) akishika kichwa baada ya kutoa 'boko' lililomzawadia goli straika wa Manchester City, Carlos Tevez (kulia) wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, kaskazini mwa England, Agosti 26, 2012. Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 2-2. Picha: REUTERS
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers na wa Manchester City, Roberto Mancini (kushoto) wakifuatilia mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, kaskazini mwa England, Agosti 26, 2012. Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 2-2. Picha: REUTERS
Mchezaji wa Liverpool, Jonjo Shelvey (kulia) akiwania mpira dhidi ya kiungo wa Manchester City, David Silva wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, kaskazini mwa England, Agosti 26, 2012. Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 2-2. Picha: REUTERS

Kiungo wa Manchester City, Yaya Toure (wa tatu kushoto) akifunga goli dhidi ya beki wa Liverpool, Sebastian Coates (kulia) na kipa Pepe Reina wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, kaskazini mwa England, Agosti 26, 2012. Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 2-2. Picha: REUTERS
Straika wa Manchester City, Carlos Tevez (kushoto) akifunga goli dhidi ya kipa wa Liverpool, Pepe Reina wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, kaskazini mwa England, Agosti 26, 2012. Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 2-2. Picha: REUTERS
Straika wa Manchester City, Carlos Tevez (wa pili kushoto) akishangilia kufunga dhidi ya kipa wa Liverpool, Pepe Reina (kushoto) wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Anfield mjini Liverpool, kaskazini mwa England, Agosti 26, 2012. Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 2-2. Picha: REUTERS
Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla (kulia) akiwania mpira dhidi ya mchezaji wa Stoke City, Geoff Cameron wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Brittania, mjini Stoke, Agosti 26, 2012. Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 0-0. Picha: REUTERS

Beki wa Stoke City, Robert Huth (kushoto) akimdhibiti beki wa  Arsenal, Per Mertesacker (katikati) na straika Olivier Giroud (kulia) wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Brittania, mjini Stoke, Agosti 26, 2012. Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 0-0. Picha: REUTERS
Straika wa Stoke City, Peter Crouch akijikunjua kuucheza mpira wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Brittania, mjini Stoke, Agosti 26, 2012. Mechi hiyo iliisha kwa sare ya 0-0. Picha: REUTERS

LONDON, England
MABINGWA Manchester City walizinduka kutoka nyuma mara mbili na kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield huku mambo yakiwa bado magumu kwa Arsenal ambayo haijaweza kufunga goli hata moja katika mechi mbili kufuatia sare nyingine ya 0-0 ugenini Britannia Stadium dhidi ya Stoke City jana.

Arsenal, ambao wamemuuza mfungaji bora wa msimu uliopita Robin van Persie kwa mahasimu Manchester United katika kipindi hiki cha usajili, walikaribia kupata goli sekunde chache kabla ya mechi kumalizika wakati mshambuliaji Mfaransa Olivier Giroud alipopiga shuti la kutokea pembeni umbali wa mita 40 ambalo hata hivyo lilipaa juu ya lango la Stoke.

Hata hivyo, angeweza kufanya vyema zaidi kama angempasia Aaron Ramsey ambaye alikuwa hana ulinzi ambaye pengine angekuwa na nafasi kubwa zaidi ya kufunga.

Stoke, ambao katika mechi yao ya kwanza walitoka sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Reading wiki iliyopita, walikaribia kufunga kupitia kwa Peter Crouch, lakini ingawa Arsenal walitawala mchezo na walifanya majaribio 16 ya kufunga dhidi ya manne ya Stoke walishindwa kuuvuka ukuta mgumu wa wenyeji.

Katika mechi iliyochezwa jioni jana, makosa mawili ya ulinzi yaliigharimu Liverpool wakati walipotoka sare ya 2-2 na mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester City kwenye Uwanja wa Anfield.

Liverpool walitangulia mbele mara mbili kupitia kwa Martin Skrtel na Luis Suarez katika mechi ya kwanza ya nyumbani kwa kocha mpya Brendan Rodgers, lakini walishindwa kulinda uongozi wao mara zote kutokana na makosa yaliyowazawadia Yaya Toure na Carlos Tevez magoli.

Inamaanisha kwamba subira ya Rodgers kupata ushindi wa kwanza akiwa na Liverpool itakwenda hadi wiki ijayo ugenini kwa Arsenal baada ya wiki iliyopita kulala 3-0 kwa West Bromwich Albion.

Baada ya kuanza hovyo, Liverpool walianza kutawala mchezo na walipaswa kupata goli la kuongoza wakati Fabio Borini alipopiga nje mpira wa krosi ya yosso mwenye umri wa miaka  17, Raheem Stirling.

Carlos Tevez alikaribia kufunga, lakini shuti lake kutokea pembeni liligonga mwamba na kurejea uwanjani.

Beki wa Manchester City, Vincent Kompany alikaribia kujifunga wakati alipojaribu kuosha mpira wa Steven Gerrard ambao ulipaa juu kidogo ya lango.

Wenyeji walipata goli walilostahili kutokana na kona, baada ya mpira uliopigwa na Gerrard kutua kwenye kichwa kisichozuilika cha Skrtel kutokea ndani ya boksi la dogo katika dakika ya 34.

Goli la kusawazisha la Man City lilikuja kinyume na mwelekeo wa mashambulizi wakati Yaya Toure alipotumia makosa ya kipa ya Pepe Reina na Martin Kelly ya kushindwa kuosha krosi ya Tevez, na kuutumbukiza mpira wavuni katika dakika ya 63.

Liverpool waliongoza tena dakika moja baadaye wakati mshambuliaji aliyecheza chini ya kiwango Suarez alipopiga 'fri-kiki' ya hatari kutokea umbali wa mita 20, kufuatia Jack Rodwell kuonekana ameunawa mpira uliopigwa na Gerrard.

Man City, ambao walizinduka kutoka nyuma na kuwafunga Southampton 3-2 wikiendi iliyopita, kwa mara nyingine walisawazisha kupitia Tevez aliyefunga bao lake la 100 katika Ligi Kuu ya England wakati Skrtel alipogeuka kutoka shujaa hadi "msaliti" kufuatia pasi yake ya kichovu ya nyuma kuibwa na Muargentina huyo aliyemlamba chenga Reina na kuutumbukiza mpira katika nyavu tupu katika dakika ya 80.

No comments:

Post a Comment