Friday, July 27, 2012

WATANZANIA KATIKA KIJIJI CHA OLIMPIKI JIJINI LONDON LEO

Baadhi ya wanamichezo wa Tanzania wakiwa na maafisa ubalozi wa Tanzania katika kijiji cha Olimpiki jijini London leo.
Viongozi wa wanamichezo wa Tanzania wanaoshiriki Olimpiki wakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe (wa pili kulia) na maafisa ubalozi wa Tanzania katika kijiji cha Olimpiki jijini London, leo.
Mtangazaji wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC), Mtanzania Charles Hilary akiwa katika kambi ya wanamichezo wa Tanzania katika kijiji cha Olimpiki jijini London leo na mmoja wa maafisa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza, Nginillah
Mmoja wa viongozi wa timu ya wanamichezo wa Tanzania akisalimiana na afisa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza katika kijiji cha Olimpiki jijini London leo.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter Kallaghe (wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Michezo nchini, Leonard Thadeo (wa pili kushoto) wakiwa na Watanzania wengine kusubiri bendera ya taifa ipandishwe katika Kijiji cha Olimpiki jijini London leo.
Hili ndilo jengo ambalo wachezaji wa timu ya Tanzania watakaa wakati wa michezo ya Olimpiki (Picha zote  kwa hisani ya Israel Saria, mdau wa issamichuzi.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment