Friday, July 27, 2012

HOILETT AJIUNGA QPR

Junior Hoilett wa Blackburn Rovers akishangilia na Yakubu baada ya kufunga goli dhidi ya Norwich City wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Ewood mjini Blackburn, England Aprili 21, 2012

Junior Hoilett

Junior Hoilett wa Blackburn Rovers akishangilia baada ya kufunga goli dhidi ya Norwich City wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Ewood mjini Blackburn, England Aprili 21, 2012

Junior Hoilett wa Blackburn Rovers akifunga goli dhidi ya Norwich City wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Carrow Road Oktoba 29, 2011 mjini Norwich, England.

'Fundi' Hoilett akichanja mbunga

QPR wamemsajili mshambuliaji wa Blackburn, Junior Hoilett kwa mkataba wa miaka minne.

Nyota huyo "fundi wa kuwapunguza na kuingia nazo" mwenye umri wa miaka 22 alifunga magoli saba katika mechi 37 msimu uliopita wakati Rovers walipoteremka daraka kutoka Ligi Kuu ya England.

Hoilett alikuwa amemaliza mkataba wake na Blackburn lakini kwa sababu ana umri wa chini ya miaka 23, QPR watatakiwa kulipa fidia. Kama pande hizo mbili hazitaafikiana ada hiyo, nyota huyo wa Canada ataenda katika mahakama ili jambo lake liamuliwe huko.

"Nina furaha sana kuwa hapa na nasubiri kwa hamu kuvaa jezi ya Rangers," aliiambia tovuti rasmi ya QPR. 

Hoilett amekuwa mchezaji wa saba kusajiliwa na Mark Hughes katika kipindi hiki cha usajili, kufuatia kutua kwa Robert Green, Ryan Nelsen, Fabio Da Silva, Ji-Sung Park, Samba Diakite na Andy Johnson.

Alikuwa akihusishwa pia na mipango ya kutimkia katika klabu ya Borussia Monchengladbach ya Bundesliga Ujerumani, lakini alichagua kubaki katika Ligi Kuu ya England.

No comments:

Post a Comment