Sunday, July 29, 2012

UBINGWA YANGA WAFICHUA UNAZI WA RAY, CLAUDI, CHALZ BABA, ALI KIBA, JAFFARAI ... WOTE NI YANGA KINOMAAAA!

Claudi aliwahi siti mapeeeeema uwanjani... hapa ilikuwa ni mishale ya saa saba na nusu hivi wakati AS Vita wakivaana na APR kumsaka mshindi wa tatu wa Kombe la Kagame jana 

Hawa Azam tutawafunga kweli? Claudi akionekana kama aliyejawa hofu vile... hapa ni kabla ya kuanza kwa mechi ya fainali ya timu yake ya Yanga dhidi ya Azam jana.
Dewji njoo Yanga tukupe cheo... baadhi ya wadau wa Yanga wakiwa na mfadhili wa zamani wa Simba, Azim Dewji (wa pili kulia) waliyemvuta na kukaa naye kwenye jukwaa lao wakati wa mechi dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana

Mimi niwashangilie nyie Yanga? Hapana, hilo haliwezekani... ! Mfadhili wa zamani wa Simba, Azim Dewji (wa tatu kulia) akiteta na baadhi ya wadau wa mahasimu wao Yanga wakati wa fainali ya Kombe la Kagame jana.   
Sehemu ya mashabiki wa Yanga waliokuwa wakiburudika na soka safi la timu yao dhidi ya Azam jana.
Kata shingo kabisa... mtoto huyu akionyesha furaha na baba yake baada ya timu wanayoishabiki ya Yanga kutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame jana.

Mtoto huyu anaendeleza mkwara wake dhidi ya wapinzani wa Yanga jana.

Muone, anashangilia kama Hamis Kiiza na Said Bahanunzi vile!
Hapa anabusu jezi ya Yanga

Anaendelea kubusu logo ya uzi wa Yanga

Msanii Vicent Kigosi 'Ray' (anayeonekana juu ya gari) akishangilia ushindi na mashabiki wenzake jana.

Ray akiendeleza shangwe na Yanga wenzake jana
Sasa ni kicheko tu... Claudi akijaidnaa kuondoka Uwanja wa Taifa baada ya kuserebuka sana na mashabiki wenzake wakati wakishangilia ushindi dhidi ya Azam. Hebu mcheki freshi, ule muonekano wa hofu kabla ya mechi uko wapi?
Chalz Baba nd'o alidatishwa kabisa kwa furaha... yeye muda wote alionekana juu ya boneti ya gari kushangilia ushindi wa chama lake.  

Yanga oyeeee! Kushoto ni Chalz Baba, kulia Ray.... wote wanashingilia ushindi na wanazi wenzao Yanga.
Mrembo huyu naye alikuwa kivutio kikubwa katika kunogesha sherehe za klabu yake ya Yanga...shavuni kajichora nini? Hayakuhusu....!

Mavuvuzela hayakutoka kirahisi mdomoni mwa mashabiki wa Yanga... si unamuona mshkaji alivyokuwa akilipuliza hadi nje ya uwanja wa Taifa baada ya Yanga kuinyamazisha Azam? Ushindi mtamu ati!

Ushindi ‘mtamu’ wa mabao 2-0 walioupata Yanga katika mechi yao ya fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya Azam jana ulifichua unazi uliopitiliza wa wasanii kadhaa nyota nchini waliofika kwenye Uwanja wa Taifa kushuhudia mechi hiyo.


Baadhi ya mastaa walioonekana uwanjani hapo ili kuishangilia Yanga na kutoka kwa uwanjani kwa furaha kubwa ni waigizaji nyota Claudi na Ray, wasanii wa bongofleva Ali Kiba na Jaffarai na pia mwanamuziki Chalz Baba wa bendi ya Mashujaa.
Aliyevutia kutokana na viwalo vyake vya kiyanga-yanga zaidi ni Claudi ambaye alitupia shati la Yanga, kofia na skafu yenye rangi ya kijani na njano ya bendera ya Yanga, huku Ray, Chalz Baba na Ali Kiba wakitupia mashati na t-shirt za Yanga. 


Jaffarai aliyeketi katika jukwaa moja na Ali Kiba na Claudi hakuvaa ‘uzi’ wa Yanga pengine kutokana na hofu ya kupata kipigo kingine kama ilivyokuwa katika mechi zao nne mfululizo zilizopita ambazo zote Yanga walitoka uwanjani kichwa chini.


Hata hivyo, Jaffarai alionekana pia akijichanganya na mashabiki wenzie wa Yanga kushangilia ushindi huo mara tu baada ya kupulizwa kwa kipyenga cha mwisho, kama walivyokuwa akina Ray, Chalz Baba , Claudi na Ali Kiba.


“Nimefurahi sana… tulionyesha soka safi sana leo na kustahili ubingwa wa michuano hii,” alisema Claudi aliyekuwa amezungukwa na mashabiki kibao wa Yanga waliokuwa wakimpigia makofi na kujaribu kumbeba.
Ray na Chalz Baba waliokuwa garini, nje ya uwanja wa Taifa, pia walijikuta wakizongwa na rundo la mashabiki wenzao wa Yanga wakati wakishangilia ubingwa wa pili mfululizo wa Kombe la Kagame.


Katika mechi hiyo, washambuliaji Hamis Kiiza na Said Bahanuzi ndio waliofunga mabao ya Yanga katika kila kipindi na kuibua shangwe na vigelegele kutoka kwa maelfu ya mashabiki wao waliofika uwanjani kuiwashangilia.

No comments:

Post a Comment